Uchaguzi 2020 Kwa mapokezi makubwa anayoyapata Lissu, chondechonde nawaomba NEC na Vyombo vyote vya Dola

Uchaguzi 2020 Kwa mapokezi makubwa anayoyapata Lissu, chondechonde nawaomba NEC na Vyombo vyote vya Dola

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,475
Nawaomba sana NEC na Vyombo vyote vya Dola, chondechonde kwa idadi ya Watanzania wanaojitokeza kumpokea na kumsikiliza Lissu kwa furaha na mapenzi yao ya dhati kwake na kwa chama chake nawaomba sana enyi watumishi wa NEC na Majeshi yetu, ruhusuni Haki ichukue mkondo wake, msiwanyime Watanzania haki yao ya kuongozwa na mtu wanaemtaka. Msiwanyime maelfu kwa mamilioni ya Watanzania furaha kwa kuwabadilishia mtu wanaemtaka na kumweka mtu wasiyemtaka.

Hata kikiingia chama kingine madarakani stahiki zenu mtapata tu, tena yaweza kuwa zaidi. Na mtu akishashindwa kihalali hawezi kuwafanya lolote,msiogope. Umati wote unaojitokeza kumlaki Lissu kuwakosesha Raha Mungu hata kaa kimya nasema.

Au maafa yakitokea kwa umati huo kuona umedhulumiwa, nyie mtapata faida gani kiuchumi na kiroho? Tazameni mapokezi ya Lissu tangu anarudi nchini na hata sasa wakati wa Kampeni,tazama Kawe,Arusha na leo Mwanza.

Kama atashindwa kihalali sawa, nyie simamieni Haki, lakini kama atashinda, mpeni Haki yake nanyi mtapata heshima ya milele na tuzo huko kwa Mungu.

Najua hata sasa hivi hatendewi Haki mtu huyu, kwa sababu hujuma juu yake Ni kubwa mno, kuliko Uchaguzi wowote uliowahi kutokea,ingawa bado watu wengi sana wanamuunga mkono.

Enyi NEC na Vyombo vya dola ruhusuni Haki itendeke.
Ni gharama nafuu mno kuruhusu Haki itendeke, lakini Ni gharama kubwa mno kuzuia Haki isitendeke.

Mkiruhusu Haki ikatendeka, mtakumbukwa Kama mashujaa wa Haki. Nayo majina yenu yataandikwa kwa wino wa dhahabu.

Vizazi vijavyo vitapenda kusoma habari zenu kwa furaha na majigambo,nayo mataifa yataja jifunza juu ya maamuzi yenu ya haki, nanyi mkiendelea kuheshimika.
 
Wengi washangaaji tu, Lissu uwezo wa kuongoza nchi hana, CHADEMA ni dhahifu sana na ikitokea siku wakaongoza watakuwa mafisadi wakubwa sana, walionesha madhaufu yao makubwa sana 2015

Mbowe ni mjanja anajua kutengeneza mazingira yenye fursa za baadae.

Anajua kuwa Lissu ni maarufu na anaweza kusaidia ongezeko la idadi ya wabunge hivyo ruzuku kuongezeka wakati wa miaka mitano ijayo.
 
Kwani mapokezi ndo kura!?...wanakukaribisha vizuri but kwenye box la kura wanakuchoma😁😁.

Note: sifungamani na chama chochote
 
Back
Top Bottom