Uchaguzi 2020 Kwa mapokezi makubwa anayoyapata Lissu, chondechonde nawaomba NEC na Vyombo vyote vya Dola

Uchaguzi 2020 Kwa mapokezi makubwa anayoyapata Lissu, chondechonde nawaomba NEC na Vyombo vyote vya Dola

Hoja yako itawafanya wakurugenzi wazidi kuengua zaidi wagombea wa udiwani na ubunge wa upinzani. Kule iringa mkurugenzi kashaengua wagombea udiwani 11 kati ya 18 wa upinzani na bado anaendelea.
 
Kuna mwanasiasa aliyepata mapokezi makubwa kumzidi Mrema wa 1995?.

Aliishia wapi?. Kama mleta mada ni mgeni kwenye siasa za TZ ni lazima utekwe na matukio ya muda tu.
Unahisi mrema hakushinda!!?Kama unazijua vizur siasa za kwetu hapa usilinganishe nyakati maana Kuna kushinda kwenye sanduku na anaetangazwa kushinda kwa mujibu wa tume.
 
Wengi washangaaji tu, Lissu uwezo wa kuongoza nchi hana, CHADEMA ni dhahifu sana na ikitokea siku wakaongoza watakuwa mafisadi wakubwa sana, walionesha madhaufu yao makubwa sana 2015
Ili mtu aongoze awe na sifa zipi kisheria?

Jee mtu anaongoza nchi kwa kufuata muongozo wa nini kisheria?
 
Kuna mwanasiasa aliyepata mapokezi makubwa kumzidi Mrema wa 1995?.

Aliishia wapi?. Kama mleta mada ni mgeni kwenye siasa za TZ ni lazima utekwe na matukio ya muda tu.
Lishalopita sio ndwele ganga lijalo.


Kwani mwanzo wakutumia simu yako ya kwanza ni hiyo iliyomkononi mwako sasahivi?
 
Kuna tofauti kati ya mapokezi na wapiga kura. Usisahau hilo tafadhali.
Uko sahihi Sana, unaweza kuona unapendwa Sana na raia kumbe ni wapambe tu wapiga vuvuzela lakini unapofika wakati wa kupiga kura ndo balaa, Kati ya watu 100 wanaopiga kura ni 30 tu
 
Kuna tofauti kati ya mapokezi na wapiga kura. Usisahau hilo tafadhali.
Hivi kama kuzungumza tuu watu hawana hamu nawe hadi Diamond au Kiba na TOT waje waimbe ndio kura watakupa kweli?

Usijidanganye, MTU hawezi kusimama juani masaa matatu kukungojea na kukusikiliza kwa furaha na asikupe kura.

Mmezoea kusema hao watu hawajajiandikisha, kwani wale milioni 29 mnaosema wamejiandikisha wanaishi wapi? Rwanda?

Siku hizi kila kijana ana kadi ya kura maana ndizo wanatumia kama vitambulisho na hata dhamana polisi mkiwakamata.
 
Jiandae kisaikolojia maana unashindwa kutofautisha umati wa watu na upigaji kura. Kimsingi kuna watu wanakwenda kwenye kampeni za Lissu kumshangaa na kucheka tu kwa vile vituko na maneno yake ya kejeli kwa Rais Magufuli na Serikali yake. Maneno anayoyaongea Lissu kimsingi ni yaleyale tu ya kejeli kejeli tu, kujiona yeye anajua sana kila kitu kumbe mweupe tu. Asilimia zaidi ya themanini ya Watanzania wapiga kura walishaamua kumpa kura JPM hilo halina mjadala na nikiangalia upande wa Wabunge Chadema inaweza kupambana labda na kupata katika Majimbo ya Mbeya Mjini, Iringa Mjini, Kawe, Bunda Mjini, Arusha Mjini, Tarime Mjini na Mikumi ila kwingineko CCM itapata viti vingi mno vya ubunge
 
Back
Top Bottom