Jiandae kisaikolojia maana unashindwa kutofautisha umati wa watu na upigaji kura. Kimsingi kuna watu wanakwenda kwenye kampeni za Lissu kumshangaa na kucheka tu kwa vile vituko na maneno yake ya kejeli kwa Rais Magufuli na Serikali yake. Maneno anayoyaongea Lissu kimsingi ni yaleyale tu ya kejeli kejeli tu, kujiona yeye anajua sana kila kitu kumbe mweupe tu. Asilimia zaidi ya themanini ya Watanzania wapiga kura walishaamua kumpa kura JPM hilo halina mjadala na nikiangalia upande wa Wabunge Chadema inaweza kupambana labda na kupata katika Majimbo ya Mbeya Mjini, Iringa Mjini, Kawe, Bunda Mjini, Arusha Mjini, Tarime Mjini na Mikumi ila kwingineko CCM itapata viti vingi mno vya ubunge