Uchaguzi 2020 Kwa mapokezi makubwa anayoyapata Lissu, chondechonde nawaomba NEC na Vyombo vyote vya Dola

Uchaguzi 2020 Kwa mapokezi makubwa anayoyapata Lissu, chondechonde nawaomba NEC na Vyombo vyote vya Dola

Huyu sio sawa na Mrema wa 1995 watu walikuwa wanamshangilia tu,mwaka huu watu wako serious
Hata Mrema 1995 kura alizipata nyingi tu. Unajua kwa nini uchaguzi ulifutwa dsm, saa sita usiku?
 
Huyu sio sawa na Mrema wa 1995 watu walikuwa wanamshangilia tu,mwaka huu watu wako serious
Hata Mrema 1995 kura alizipata nyingi tu. Unajua kwa nini uchaguzi ulifutwa dsm, saa sita usiku?
 
TBC pia warushe baadhi ya mikutano yake live ili wananchi waone kisha wapime. Kama wananchi wanaona tu ile ya ccm watajiuliza kwa nini na hiyo wasifikiri kwamba ni faida kwa ccm, la inaweza kuwa ni hasara.
 
Nimeelewa sana hoja yako.


Kwamba HAKI isimamiwe na vyombo vinavyohusika katika uchaguzi huu yaani (NEC) pamoja na vyombo vya dola.


NEC hawako tayari kusimamia haki maana wanapokea maagizo ya CCM, hili ni tatizo kubwa.


Mimi naomba JWTZ (CDF) na Polisi (IGP) waingilie kati na kushurutisha kila mhusika kwa nafasi yake atende HAKI, yaani:

1. NEC ishurutishe kusimamia uchaguzi bila upendeleo wote

2. Polisi walinde kwa HAKI bila kujihusisha na uporaji wa masanduku ya kura, Wasiwakamate na kuwatia ndani mawakala wa vyama vya upinzani ndani; ili kutoa mwacha wa kupora ushindi;

3. Wasimamizi wa uchaguzi washurutishwe kutenda HAKI na watakaobainika kuvuruga na kupendelea washtakiwe mara moja kwenye mahakama ya kijeshi;

4. Wagombea wote ambao bado wanayo madaraka ya kiserikali wasijihusishe kwa namna yoyote kutoa amri kwa vyombo vinavyosimamia uchaguzi

5. Wapiga kura waruhusiwe kushuhudia uhesabuji na utangazaji wa matikeo ya uchaguzi katika vituo vyao;

Endapo CDF na IGP watasimamia yote hapo juu, HAKIKA ile fahirisi ya furaha (hapiness index) ya nchi yetu inaongezeka maradufu na vyombo vyetu hivyo vitapata HESHMA kubwa. Aidha, wakuu wa vyombo hivyo watakuwa wamejiwekea historia mbayo haitakaa ifutike katika nchi yetu.

Mungu Ibariki Tanzania, MUNGU wape ujasiri CDF na IGP pamoja na watendaji wote wa vyombo wanavyoviongoza ili waingilie kati uchaguzi huu.

Wasalaam,
Ngilenengo
 
Kuna tofauti kati ya mapokezi na wapiga kura. Usisahau hilo tafadhali.
kisingizio cha kuwa vijana sio wapiga kura sasa juzi segerea kulikua na makundi yote vijana na wazee na wa lika la kati,CCM isije anza kutumia marungu bwana watu wanahasira na miaka mitano iliyopita.Kwetu wanasema umeme umefika lakini ukifika pale unajiuliza kipi kilikua bora katika kipindi cha kikwete na Profesa Muhongo waliosambaza vijiji 2000 vya mwanzo lakini hawakua wanafanya piloting style kama ilivyosasa ya kupitisha umeme kijiji kizima transform moja na kitongoji kimoja kwa heri.
 
Tatizo ninyi hamtaki kuambiwa ukweli siyo anayeenda kumsikiliza Lissu au Magufuli ndo atawapigia kura wengine ni mamluki tu.
Lakini wapiga kura si ni hawa hawa wananchi ?!. Au wapiga kura ni malaika ?
 
Wengi washangaaji tu, Lissu uwezo wa kuongoza nchi hana, CHADEMA ni dhahifu sana na ikitokea siku wakaongoza watakuwa mafisadi wakubwa sana, walionesha madhaufu yao makubwa sana 2015
Nchi inaongozwa kwa katiba na sheria kupiti mifumo thabiti na vyombo tasii zilizojengwa imar. Nchi inayomtegemea mtu mmoja lazima shida iwepo. Lisu amezungumzia suala la katiba na mifimo imara. Hili ndilo muhimu. Hizi sio enzi za mitume

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Kuna tofauti kati ya mapokezi na wapiga kura. Usisahau hilo tafadhali.

kama ndivyo kwa nini CCM ameanza kumtaka Mh. Lissu amwachie nafasi ya urais kwa ahadi ya kumpatia "uteuzi" kama akishinda?
Kudaddeki alizoea kuwahonga vyeo akina Molleli,Kitilya nk na washamba wenzake wa CCM ili awale sasa kwa Mh.Lissu ni mwisho wa mambo yake ya kishamba.
 
Ninatafakari kidogo. Huu umati wa mikutano ya kampeni vyama vya upinzani,hususani CHADEMA,wanafuata nini. Wasanii wote wakubwa(muziki,comedies,filamu nk) wako CCM. Watu makini huhudhuria mikutano ya wapinzani,wanataka kusikia ladha tofauti ya siasa,majibu ya ugumu wa maisha tofauti na inavyohubiriwa kwenye kampeni za CCM(stieglers,madege,sgr,maboma ya vituo vya afya ambayo hakuna dawa wala watumishi..madaraja) huku watu hawana ndururu,njaa,madeni kila kona,biashara zimedoda. Nafikiri wanaohudhuria mikutano ya wapinzani ni serious people,wapiga kura.
 
Makada wa NEC wanachaguliwa na Rais.. unafikiri watamvusha mtu baki waingie hatiani.. NEC NI YACCM HAKUNAGA TUME HURU AFRICA
 
Watu wapo tayari kwa ajili ya mabadiliko , hasa katika box . kundi hili ni vijana na waliomaliza vyuo na wale wasio na ajira . kundi la wafanya biashara na hasa ambao katika utawala huu hawajaguswa . Wanawaza bwana mkubwa aendelee tu na hasa wale wenye maslahi na chama au serikali .

Kundi lilikuwa kubwa linalotaka kujua huyu akija atasema nini , mi mean tundu lissu . Kwa sasa naona hilo kundi linakuja kwa kasi kukubali sera na maneno ya upinzani .

Kufungiwa siasa kwa kipindi cha miaka mitano kulikuwa kuzuri na kubaya . kwani watu wangeelewa mapema leo mikutano ya chama tawala ingekuwa na watu wa chama husika tu na wala si ya wote .

Maendeleo ya vitu na watu . chama tawala wanashindwa kuvielezea ipasavyo . hata kuleta mashiko kwa watu . ila ninachoona kwa sasa ni watanzania wengi , wanawaza hivi hata huyo lissu akiingia itakuwaje ? . wapo in dillema , kutokana na ukubwa na mikakati ya chama tawala

Wengi wanabaki na maneno ya jumla jumla . ''' hata akishinda hatateuliwa ''. ccm hawatakubali.

Ningeshauri watanzania kuna msingi sana wakutoa haki na kuombea taifa , ili tuweze kufika tuendako .
 
Halafu miaka.5 sio mingi akibebes tunammwaga chini
emoji109.png
emoji107.png
 
Back
Top Bottom