Kwa mara nyingine, Asante JamiiForums

Kwa mara nyingine, Asante JamiiForums

F4B

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2022
Posts
336
Reaction score
429
Napenda kutoa shukrani zangu kwa jukwaa hili hasa members kwa jinsi mnavyo changia mijadala mbalimbali. Kwa namna ya pekee naushukuru uongozi wa jukwaa hili.

Kwa mara nyingine tena nilileta humu KERO fulani na ikatatuliwa.

Ikumbukwe Jana nilileta habari ya makarani kunyanyaswa na viongozi wa ngazi za mkoa na wilaya katika baadhi ya maeneo ya nchi yetu.

Habari husika >> Usalama wa Taifa saidieni kumpa Rais Samia taarifa sahihi

Naomba ieleweka kuwa serikali ilishatoa fedha zilikuwepo maeneo hayo ila ukiritimba ulipelekea wakarani kunyanyasika. Lakini habari hiyo nilipoiposti humu muda mfupi baadaye pressure ilikuwa kubwa mno kwa waratibu wa sensa wilaya na Kwa Wakurungenzi hatimaye makarani maeneo korofi karibu yote walipata fedha zao.

"Asante JamiiForums, information is power"
 
Mkuu, karani mmoja wana dada aliingia siku zake ghafla akaenda badili bahati mbaya alichobadili kikanasa maliwatoni na maliwato ikaziba. Makarani WA kike wakatozwa mia Tano wapo mia moja ili kuzibua choo.

Baada ya Mimi kutupia humu walirudishiwa pesa Yao na kuombwa radhi.

Asante JF
Ulifanya jambo jema sana. Huu ndo UTU
 
Jf is the home of great thinkers..humu kila viongozi wa mkuu wa hii nchi wamo..wawe wa kisiasa..kiusalama wote wamo huwa wanachungulia.

Mengi wanayajua na mengi wanayafanyia kazi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hakika, humu kero hua zinasomwa na wote, haswa viongozi...
 
Back
Top Bottom