Kwa mara ya kwanza nimefika Mwanza nimekutana na stand Mpya ya Nyegezi. Hayati Magufuli CCM ilipoteza Rais!

Mambo mengine niyakawaida.yanachelewa kufanyika kwasababu yakua na serikali iliyochoka madarakani.Fedha zinazopatikana nchi hii tungekua na uongozi makini nchi ingekua mbali sana.Leo tunashangaa ya Jpm kwasababu tumezoea maendeleo kwetu ni anasa.Kwakua Jpm alikua mmoja na leo hayupo wananchi wana kila sababu yakuamka nakujua kua kumbe mambo makubwa na mazuri yanawezekana endapo tutaamua kua na viongozi wanaojielewa.
 
asingekuwa mkatili, alikuwa mtu mtendaji sana, na ninaamini miaka ya mbeleni tutamhitaji rais kama yule ila apunguze ukatili kidogo.
 
Kwa sasa ameshatutoka! Tumwombe Mungu 2025 atupe Rais atakayekuwa na moyo wa kizalendo wa Hayati, ingawa kumpata mtu wa aina hiyo ni kazi kweli kweli.
 
Ngosha karibu mwanzaaa....jmosi uje hapa bambino turuke nyokaa
 
Safi sana kaka .
Ukipata muda usiache kufika hapo Makoroboi uone uumbaji wa Mungu pia
 
Majizi yamerudi jikoni, kumpata tena mtu kama JPM wa kuyadhibiti ni swala la majaliwa ya mola.
 
Ukitaja jina la Magufuli unatonesha donda bichi kwenye mioyo ya watu, Kila siku nchi inamlilia Kwa mazuri mengi aliyotenda.

Yawezekana baadaye neno Magufuli likaongezwa na BAKITA kwenye kamusi likimaanisha mzalendo, mpambanaji na mfia nchi.
 
Ni kweli, stendi zote mbili: Nyamhongolo na Nyegezi ni nzuri sana.

Mwezi August 2023 nilipita hapo Nyegezi.

Lakini pamoja na uzuri wake, nina mashaka uzuri uliopo unaweza kupungua sana baada ya muda mfupi kutokana na upungufu wa ustaarabu.

Ni miezi michache tu imepita tokea ilipofunguliwa, lakini vyoo vimeshaanza kuharibika kwa kuharibiwa. Inasikitisha sana.

Pengine, ingetolewa "semina" ya jinsi ya kutumia vyoo vya kisasa.

Kwa hali niliyoishuhudia, inaonekana bado kuna changamoto kwenye namna bora ya utumiaji wa vyoo vya kisasa.

Siku hiyo niliwauliza wahudumu wa hivyo vyoo kwamba kwa nini wasiwe wanawaelekeza watu jinsi ya kuvitumia, wakasema wengine ni wabishi. Wakielekezwa jinsi ya kuvitumia, husema wanajua. Lakini muda mfupi baadaye, ukiingia unakuta kuna kifaa kimeshaharibiwa. Mpaka wengine wanatamani askari wa JKT wapewe jukumu la kuvisimamia kwa muda mpaka watu watakapovizoea.

Kama tahadhari haitachukuliwa, baadhi ya miundombinu, hasa ya upande wa vyoo, itaharibika kabisa, baada ya muda mfupi.
 
Tuko timu ya watanganyika tunazunguka nchi nzima kuangalia miradi iliyoanzishwa na Hayati magufuli Ili kuwaeleza na kuwaambia CCM sifa za Rais tu naye mtarajiwa 2025.[emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064]

Mmh kwani mna hakika CCM itashinda uchaguzi?[emoji848][emoji2827]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli was Gifted, Nikiangalia SGR haieleweki inaanza lini namkumbuka sana Mzee uyu
 
Aise apewe pongezi zake
Itabidi dada yangu FaizaFoxy
Afike hapo atembe [emoji1]

Ova
 
Mkuu nakushauri fika na kivukoni,kigongo-busisi. Hujasema mpaka useme.
CHADEMA MADE ME TO HATE MAGUFULI,am sorry for that. NOW I HATE CHADEMA AND ALL ANTI-MAGUFULISM FROM ccm. Tulimpoteza Rais wa kweli kwa siasa mbovu na ufisadi uliokitiri.

Na atasema[emoji28][emoji28]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…