Ninarudia kusema CCM kumpoteza Magufuli ili pata hasara ya Karne moja.
Nyegezi kulikuwa Bondeni na eneo lisilofaa leo nimekuta kifaa kama airport.
Magufuli Ulifanya kazi nzuri tutakukumbuka.
Bado ninasikia kuna stand nyingine Huku Mwanza imejengwa na Magufuli Ndio ninaelekea huko kuangalia. Nikifika Nitakujulisha niliyoyakuta ila CCM ilipoteza Rais Kwa kweli.
Tutatembelea bandari ya Mwanza, Meli alizozijenga, uwanja wa ndege wa Mwanza na mradi wa SGR Mwanza kwenda Isaka.
Mwisho nitatembelea daraja la kigongo busisi na Nitapiga picha!
Tuko timu ya watanganyika tunazunguka nchi nzima kuangalia miradi iliyoanzishwa na Hayati magufuli Ili kuwaeleza na kuwaambia CCM sifa za Rais tu naye mtarajiwa 2025.
Ni kweli, stendi zote mbili: Nyamhongolo na Nyegezi ni nzuri sana.
Mwezi August 2023 nilipita hapo Nyegezi.
Lakini pamoja na uzuri wake, nina mashaka uzuri uliopo unaweza kupungua sana baada ya muda mfupi kutokana na upungufu wa ustaarabu.
Ni miezi michache tu imepita tokea ilipofunguliwa, lakini vyoo vimeshaanza kuharibika kwa kuharibiwa. Inasikitisha sana.
Pengine, ingetolewa "semina" ya jinsi ya kutumia vyoo vya kisasa.
Kwa hali niliyoishuhudia, inaonekana bado kuna changamoto kwenye namna bora ya utumiaji wa vyoo vya kisasa.
Siku hiyo niliwauliza wahudumu wa hivyo vyoo kwamba kwa nini wasiwe wanawaelekeza watu jinsi ya kuvitumia, wakasema wengine ni wabishi. Wakielekezwa jinsi ya kuvitumia, husema wanajua. Lakini muda mfupi baadaye, ukiingia unakuta kuna kifaa kimeshaharibiwa. Mpaka wengine wanatamani askari wa JKT wapewe jukumu la kuvisimamia kwa muda mpaka watu watakapovizoea.
Kama tahadhari haitachukuliwa, baadhi ya miundombinu, hasa ya upande wa vyoo, itaharibika kabisa, baada ya muda mfupi.