Kwa mara ya kwanza nimehisi kuwa na umuhimu

THECODONT

Member
Joined
Mar 11, 2022
Posts
99
Reaction score
302
Baada ya kumaliza Chuo mwaka jana life ikapiga vibaya mno, kila muda nilikuwa nawaza jinsi gani nitasaidia familia yangu (Ni mtoto wa kiume mkubwa) Ilikuwa inauma sana pale ambapo unaamka asubuhi huna cha kufanya hadi kuna muda unahisi kama kifua kinabana.

Kuna muda nakaa najitafakari naona kama ni mzigo home, but hakuna aliyewahi niambia, sister kuna muda mshahara ukitoka ananitoa laki basi maisha yanaenda.

Mwanzoni mwa mwaka huu kuna mchongo nikaupata katika harakati za kushughulikia ili utiki, nikawa naingia katika mzozo sana na mzee maana mara nyingi nilikuwa narudi usiku anamind, ananisema ila kwa upande wangu inaniuma lakini nakaza ili isionekane kama imeuma (akaanza kuona kama namdharau) sasa kuna muda huna nauli kuomba siwezi so nachukua bike kutoka home hadi kwenye michakato as usual narudi usiku.

Kwenye kuhangaika hivyo mchongo ukatiki nikatumiwa mkataba nikasign nikaenda kazini, nikaona afadhali nimetoka home, mchongo unalipa fresh tu, silipi kodi wala bills kama maji, umeme na utilities zingine, na ni apartment nzuri unyama ni mwingi.

Leo account imesoma kwa newhires wote mzigo umesoma almost M 8, nikatoa M2 nimewatumia home, bi mkubwa ameshukuru mnooo, kuna ile feeling ya kuwa Now na wewe ni wa muhimu, sijawahi jisikia vizuri kama leo, ameninenea maneno ya Baraka hadi nikahisi zinajaa physically. Leo na mimi nimehisi ni wa muhimu.
 
Hongera mkuu
 
Wakati mwing
Wakati mwingine hadithi kama hizi huwa zinamriwaza mtu!! unajitungia hadithi nzuri angalau ikutie moyo huku ukiomba siku moja iwe kweli!! Ila hata kama ni hadithi, ungejaribu kuipa uhalisia kidogo!! hapo kwenye M8 bongo hii umechapia sana!! Kama ni upigaji sawa!! lakini new hire??? jaribu kutunga kwa uhalisia wakati mwingine!!
 
Huyo sister aliyekupa laki, mtumie hata laki 3 km shukrani.
Usimsahau aisee
 
Mzee kahangaika sana kutafuta pesa za kuwasomesha na kuwalisha ila mtoto akipata anaekumbukwa ni Mama, DUH!!

Pesa ilibid umtumie aliekuwa na majukumu yakuwatafutia pesa (baba), mama nae akipewa anashukuru.

Hii na wewe inaweza kukurudia ukipata watoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…