Kwa mara ya kwanza ulipopata taarifa ya kifo cha J.k Nyerere ulijisikiaje?

Kwa mara ya kwanza ulipopata taarifa ya kifo cha J.k Nyerere ulijisikiaje?

Mimi nilikua chekechea basi mwalimu akatuambia kua baba wa taifa Mwl. Nyerere katutoka hivyo tunatakiwa tuende nyumbani.Basi wakati wa kurudi nyumbani barabarani kukawa na makundi ya watu wanaongelea kifo chake.Wengine wakawa hawaamini.. dah!
 
Mimi nilikua chekechea basi mwalimu akatuambia kua baba wa taifa Mwl. Nyerere katutoka hivyo tunatakiwa tuende nyumbani.Basi wakati wa kurudi nyumbani barabarani kukawa na makundi ya watu wanaongelea kifo chake.Wengine wakawa hawaamini.. dah!

Kumbe bado mdogo sana ila hyo picha uliyoiweka unaonekana mrembo sana
 
Nakumbuka tulikuwa kijiweni na rafki zangu mida ya saa NNE asubuhi Mzee Mkapa akitumia RTD kutangaza kifo cha nyerere, Mzee mmoja akasema vijana Nyerere kafariki hamjala nchi bado, basis nilihuzunika nikijua bila Nyerere huenda nisingeishi vizur, kumbe maisha huendelea hata kipenzi chako akifariki
 
....nilipata faraja kubwa.....kiukweli namchukia huyu kafiri...
Wewe ulishafanya kufuru ngapi tangu upate akili? Kitabu chake kishafungwa,chako unajuwa kitaandikwa nini? Unamchukia kwani ulimuumba wewe?
Usipende kujilaani,nimeshuhudia wengi wenye nafsi kama ya kwako wakiwa bado malofa na huwa wanalalamika na kulaani kama wewe.Nyerere alikuwa ni binadamu kama wengine,madhaifu yake yapo.Ila angalia unapotoa hukumu kama hiyo,jikague kwanza una ucha Mungu?Isiwe kuvaa kanzu na bargashia ili uonekane na watu iwe ndiyo sababu ya kuwaita wenzio makafiri.Kwanza Qur'an inakataza tusiitane majina mabaya.inawezekana hukumu uliyompa Mzee huyo ikawa tofauti na unavyotaka iwe.Mungu ndiye mjuzi
 
nilikuwa Darasa la pili..mdogo mdogo enzi hizo ila mtundu balaa...alivyokufa mgalatia nilikuwa home tu nisharudi toka shule nilifurahi kichizi pale mam aliponiambia hatutoenda shule mpaka azikwe na msiba upite

#Zitto
 
Nilihuzunishwa sana na kifo cha Mwalimu Nyerere, nilipenda kusikiliza hotuba zake katika ule umri wangu mdogo, Mwalimu Nyerere ni mwanadamu kama wanadamu wengine ana mazuri na mabaya yake ila alifanya mengi kwa nia nzuri hata yale mabaya aliyoyafanya ilikuwa kwa lengo jema, tumkumbuke kwa yale mema aliyotenda na tumsamehe kwa yale mabaya aliyotenda ila binafsi naamini Mwalimu alikuwa jembe la ukweli alichukia rushwa kwa dhati toka moyoni mwake hilo halina pingamizi kwamba alikuwa hapendi rushwa
 
Nilikuwa darasa la pili. Niliambiwa baada ya kifo chake vita inakuja...niliogopa sana. Nilikuwa sijakomaa ufahamu vizuri.
 
MI NILIJISIKIA KAWAIDA KAMA WENGINE WANAVYO KUFA sikulia nilisikitika tu kwakuwa ni binadam mwenzangu lakn namchukia kupita maelezo na nikisikia tu jina lake napata kichefuchefu alaf nahis kizunguzungu
....nilipata faraja kubwa.....kiukweli namchukia huyu kafiri...
kukupigania wewe na ukoo wenu kwa ujumla muwe huru katika nchi huru na si koloni la kiingereza ndo sababu ya wewe kumuita kafiri ama kumchukia....
 
ingawa watu walishakata tamaa kwa ugonjwa wa mwalimu siku hiyo ilikuwa kama mzizimo fulani. kwa muda mfupi ilikuwa kimyaaa. watu walikuwa kama wamepigwa na bumbuwazi. mimi nilishtuka haikuwa kawaida kwa kweli
 
Nakumbuka nilikuwa nje ya nchi ilikuwa mida ya saa tano hivi nilikuwa library katika kuchagua gazette moja wapo mbele ni habari yake. sikushtuka sana kwani condition aliyokuwa nayo before ilikuwa inajieleza.
 
Back
Top Bottom