Kwa Mara ya Mwisho nimeamua kuwa support CHADEMA, Watanzania wenzangu 2025 ni Mwaka wa kujisahihisha "say NO to CCM"

RNA

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2013
Posts
1,647
Reaction score
2,803
Habari jf ,kwanza niweke Wazi Mimi ni mfuasi wa lile kundi linalosemwa vibaya la Hayati JPM na msimamo wangu utabaki pale pale ndiye best president to rule this country .

CHADEMA kiuhalisia ukiwatoa Wilbroad slaa na Tundu Lissu hakuna kiongozi aliyewahi kuwa serious na kuchukua Nchi ,ni huwa wanaingiza mtu kugombea au anagombea Mwenyekiti kama ushahidi tu .

Hivyo Kwa akili yangu timamu 2025 mbali na kuwa na dalili :-
1.Mwenyekiti Mbowe kuwa hana makali tena kutokana na makubaliano ya maridhiano

2.Nafasi zilizopo ni upande wa ubunge na madiwani upande wa Urais hakuna namna

Nitakuwa upande wa chama changu CHADEMA na nitashawishi wananchi wengine wakiunge ili tuweze chukua dola na sio wabunge maana 2025 nafasi iko Wazi .

Wananchi tuwasamehe CHADEMA na tuwaunge mkono tena .

"Say NO to CCM "Uwezo wao tushaujua hautoshi kutuletea maendeleo .

Tusisahau Katiba MPYA sio jambo la kuombwa na la CHADEMA peke yake ni jambo la kila MTU tuungane ipatikane .
 
Mh ngoja waje wenzako tuone wanasemaje!!
 
Unawasapoti Kwa yapi mazuri Yao, au ni Kwa kupambana na alieko kifuani mwa ibrahimuu??
 
Mwanaccm maji yamekufika shingoni. Hongera kwa wokovu
 
Wanaoamini ktk MAZURI ya Magu wapokelewe CDM?

Sijui kama inawezekana, Mbowe Juzi tu huko kusini kamtukana tena mfu na akazomewa na wananchi mkutanoni.

Unaonaje tukipambania KATIBA mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA,

Urais tusimamishe MGOMBEA binafsi asiyetokana na vyama vya siasa?
 
Ondoa najisi yako CHADEMA usije leta mikosi. Mtu yeyote aliyekuwa mfuasi wa Magufuli kwa kweli hastahili kwenda CHADEMA.

Magufuli ametesa, ameua wana CDM na alitaka kukifuta chama kwenye ramani ya vyama vya siasa. RNA tafuta mahali pengine lakini CDM nimekataza, utatunajisi
 
Uongo huo. Mbowe alizomewa wapi?
 
Kuna msamaha jamii itawasamehe lakini walifanya vibaya.
 
RNA anasafishika, mbona LOWWASSA mkt alimsafisha?

Mbona Juzi Mbowwee kawapokea wafuasi wa Lipumbawe?

Acha nongwa.
 
Japo kama umechanganya kachumbari na mchanga ,lakini nimekuelewa chama cha kuwaletea watanzania maendeleo ya kweli ni Chadema hivyo tuwaunge mkono na tuwasaidie wengine kutambua hilo.Kataa CCM
 
 
Nimemsikia mm Kuna muda mbowwe kazomewa mkutanoni Hadi akanyamaza akasema TULIAAAA Kisha akaendelea kumtukana Magu.

Nawauliza CDM na mbowwe,

Kwani ni LAZIMA Kila mkt akishika mike lazima Amshukuru Sa100 na kumtusi Magu?

Nauliza kwani ni LAZIMA?

Tangu lini Mpinzani Kila mkutano anashukuru Serikali kabla ya kuhutubia wananchi?

Badilikeni.

Mtachokwa mapema. Yaani mnakuwa kama TLP ya Mzee Mrema enzi za Magu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…