Alfred
JF-Expert Member
- Apr 13, 2008
- 2,093
- 2,843
Mtumishi wa Mungu Dada na Mama yetu Sr. Suzan Barthlomeo amefariki dunia kwa tukio linaloaminika kujirusha toka Ghorofani baada ya Misa za Asubuhi!
Kikatoliki si Halali kwa Marehemu kufanyiwa ibada za Mazishi endapo Kifo chake kimetokana na Kujiua (suicide)!
ila Kwa Marekebisho haya ya Sheria za Kanisa (Canon Laws) Tusishangae kuona Sr. Akizikwa kwa taratibu na ibada zote zinazostahili (na iwe hivi)!
Canon inasemaje? Tureje Kidogo Kuhusu Sheria za Kanisa Kuhusu Misiba! (Hapa nitazungumzia Case ya Mtawa Huyu Ambayo itamtetea)
Can. 1184
. Isipokuwa walitoa ishara za toba kabla ya kifo, Case zifuatazo lazima zizuiwe katika mazishi ya kidini:
1 / sifa mbaya, wasioamini
2 / wale waliochagua kuungua kwa miili yao kwa sababu za kinyume na imani ya Kikristu;
3 / wengine wenye dhambi dhahiri ambao hawawezi kupewa mazishi ya kanisa bila ya kashfa ya watu waaminifu.
§2. Ikiwa shaka yoyote hutokea (labda kuhusu kifo kilivyotokea au hali ya marehemu kabla ya kufa) Mashauriano yafanyike kama marehemu atapatiwa ibada ya mazishi au la!
Hayo Maandishi ya Blue, Case ya Mtawa huyu itaangukia Hapa (Mark my words) na atazikwa kwa taratibu zote zinazofaa na heshima Kubwa tu!
Pumzika kwa Amani sr. Suzan Bathlomeo!
ALFRED