Kwa matokeo haya atasoma chuo kikuu??????

Bendera ya Bati

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2011
Posts
279
Reaction score
369
Ndugu yangu kapata matokeo yake ya kidato cha sita,amepata div.3 ya 14 katika combination ya HGK (E,E,D) Sasa je anaweza kusoma elimu ya juu hususani degree?na je yuko eligible kuomba mkopo?
Wasiwasi wake anahofia kuingia gharama ya 60,000/= alafu ikala kwake.Msaada wa mawazo kutoka kwenu utamsaidia sana.
 
Anaweza kuapply most facult za Baed na loan akapata hata 100%. Awe care na vyuo vya kuomba.
 
anaweza kusoma kwenye hivi vya kata! UD sidhani kama inawezekana!
 
vya kata kama? i thought now TCU is regulating the selection,that to be admitted to any university u shd possess agiven qualification!
 
Mimi mdogo wangu ana Three ya 17,HGL(fde) atapata chuo jamani? Msaada please!!!
 
Kwa matokeo yake anatakiwa kuomba kusoma kozi yoyote ya ualimu na atapata bila shaka na mkopo juu.
akiomba kozi tofauti na ualimu kupata ni bahati nasibu na mkopo hawezi pata.
Huo ndio uhalisia,uamuzi ni wenu.
 
ukiwa na div 3 chuo anaweza pata kozi za ualimu na mkopo atapata pia.
kozi nyingine kupata ni ngumu na mkopo asahau.
 
kwa kubahatisha anaweza kuomba course tofauti na kupata, ila kwa uhakika ni education na full mkopo
 
Kwakweli ni ngumu sana, angalau ingekuwa science kidogo, tena mwaka huu inaonekana form 6 wamefaulu vzuri. Hapo inabidi achague kwa makini chuo na kozi pia. TCU wanakuwa na vigezo vya jumla na vigezo vya kila chuo, so aangalie vigezo (wakati wenzake wana-apply) kabla hajalipia. Ajaribu education mkwawa na udom-ambavyo vinachukua wanafunzi wengi. Pia kuna saut-mtwara.
 
Ndugu yangu kapata matokeo yake ya kidato cha sita,amepata div.3 ya 14 katika combination ya HGK .

Mimi mdogo wangu ana Three ya 17,HGL(fde) atapata chuo jamani? Msaada please!!!
Wakuu bila kuwaficha haya matokeo kwenda versity ni ngumu labda muwe na marefa wa maana sana. Labda waende diploma kisha wataunganisha, otherwise ni ngumu. Siwakatishi tamaa ila nawaeleza ukweli ili msiwe na false hopes!
 
vya kata kama? i thought now TCU is regulating the selection,that to be admitted to any university u shd possess agiven qualification!
Licha ya TCU ku-regulate, kila chuo kina cut-off point zake! Ndiyo maana unaweza kukuta UD wakamkataa Mzumbe wakamchukua au IFM, this is natural you don't have to argue about!
 
Wakuu bila kuwaficha haya matokeo kwenda versity ni ngumu labda muwe na marefa wa maana sana. Labda waende diploma kisha wataunganisha, otherwise ni ngumu. Siwakatishi tamaa ila nawaeleza ukweli ili msiwe na false hopes!
Ila hapa bongo usijeshangaa ukamkuta ka-join kwa hizo hizo points! Bongo njia zipo nyingi!!!!!
 
Kwa matokeo yake anatakiwa kuomba kusoma kozi yoyote ya ualimu na atapata bila shaka na mkopo juu.
akiomba kozi tofauti na ualimu kupata ni bahati nasibu na mkopo hawezi pata.
Huo ndio uhalisia,uamuzi ni wenu.

Mkuu inaonekana kama vile unaidharau fani ya ualimu. Sasa huyo akienda kusoma ualimu awe mwalimu utakubali aje kundisha mtoto wako? Naye kapata lower grades b'se inawezekana walimu waliomfundisha nao walikimbilia ualimu baada ya kupata grade za chini. Bora kuiheshimu hii fani ya ualimu kama tunataka kuepukana na grade mbaya. Utaniambia ndio tulivyo watanzania lakini inabidi tubadilike kwa kweli. Tuheshimu fani ya uliamu. Labda utaniambia asomee ualimu halafu atabadilisha fani huko mbele, lakini wakati akisubiri kubadalisha fani atakuwa tayari ameshafelisha wangapi?

By the way, kwani yeye anataka kusoma ualimu. Let him/her pursue his/her dream. Kama ana dream but qualifications hana then arudie. Sioni kama ni vizuri kumshari mtu akasomee ualimu wakati hiyo fani haipo kichwani kwake. Kama dream yake ni kuwa mwalimu then, let him do that.
 
Mheshimiwa kwani hujui kwamba bongo nafasi za Ualimu, Upolisi, Jeshi na manesi wa hospitali ndo zimeachwa kama last resort ya lower grades? Sijui aliyeasisi huu mwelekeo!
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Mkuu inaonekana kama vile unaidharau fani ya ualimu. Sasa huyo akienda kusoma ualimu awe mwalimu utakubali aje kundisha mtoto wako? Naye kapata lower grades b'se inawezekana walimu waliomfundisha nao walikimbilia ualimu baada ya kupata grade za chini. Bora kuiheshimu hii fani ya ualimu kama tunataka kuepukana na grade mbaya. Utaniambia ndio tulivyo watanzania lakini inabidi tubadilike kwa kweli. Tuheshimu fani ya uliamu. Labda utaniambia asomee ualimu halafu atabadilisha fani huko mbele, lakini wakati akisubiri kubadalisha fani atakuwa tayari ameshafelisha wangapi?

By the way, kwani yeye anataka kusoma ualimu. Let him/her pursue his/her dream. Kama ana dream but qualifications hana then arudie. Sioni kama ni vizuri kumshari mtu akasomee ualimu wakati hiyo fani haipo kichwani kwake. Kama dream yake ni kuwa mwalimu then, let him do that.

Nadhani hujanielewa mkuu...hoja yangu hapa ni kwamba kwa matokeo ya division three ni ngumu kupata udahili kwa kozi nyingine zaidi ya ualimu.
nimejaribu kutoa uhalisia wa mambo na si kuonesha dharau kwa fani ya ualimu.
anaweza bahatisha kupata udahili kwenye kozi tofauti na ualimu ila sera ya serikali ni kwamba walio eligible kupata mkopo ni waliopata div 1 na 2 bila kujali unasoma kozi gani na div 3 kwa wanaosoma ualimu.
dhambi yangu kama ipo kwenye kutoa taarifa hapo nitakubali mkuu
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Back
Top Bottom