Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,734
- 5,750
Nani anapenda kumzika ndugu yake ambaye amepoteza uhai kabla Mungu hajamuita. Mbaya zaidi wanaokuwa wamemuua hawachuliwa hatua kisheria.
Kila siku kukicha tunasikia vyombo habari watuhumiwa kujinyonga selo za polisi katika mazingira ambayo tafakuri ikifanyika watu hawapati majibu.
Tukio la binti anayeeleza kuwa baba yake alivuliwa nguo mbele yake kisha na yeye binti kulazimishwa kuvua ili alale na binti yake ni kinyume cha haki za binadamu na hata katiba ya JMT. Ibara ya 12(1) ya katiba ya JMT ipo wazi kabisa kuwa kila Mtanzania ana haki ya kuheshimiwa utu wake.
Sasa kama katiba inapindishwa na wananchi hatuna mamlaka juu ya kudai haki zetu kwa nini tuwe na katiba ya hivi.
Tuwe na katiba ambayo itatumpa mamlaka ya kudai haki zetu iwapo ndugu zetu wanauawa na watu ambao hawachukuliwi hatua.
Mwaka huu tupate katiba mpya ili tudai haki zetu.