Wenye hekima, wale wa juu juu, wasiofahamu chadema kwa kina, chawa wa mitandaoni, nadhani wamepata ufunuo hasa kwa undani juu ya kwa nini mbowe anastahili kuendelea kuwa mwenyekiti, kuna wakati ulika chadema ikawa chungu, na wale majasiri njaa wakapatwa na woga mkali wakaona wayaokoe maisha yao kwa kutimua mbio ughaibuni,
#swala la msingi tujiulize je hawa watimua mbio wanatustahili?, kuwaachia chama?.
Napata sana mashaka!
Mbowe dili lake kubwa ni kutoa siri kwa vyombo vya dola juu ya nani msumbufu ili ashughulikiwe kisawasawa.
Magufuli hakuwa mnafiki ndio maana alitaka kukifutilia mbali chama cha Familia ya Mbowe .
Mbowe ni mpumbavu kwa sababu amemuharibia kabisa ndoto ya mtoto wake ndani ya chama. Kwa sasa mtoto wa Mbowe hawezi kuja kuaminika na kupata nafasi ya kuchaguliwa kwa sababu ya udikteta wa baba yake.
Mbowe alikua na nafasi kubwa sana ya kumjengea jina zuri mtoto wake kwa wananchi . Madikteta wote duniani hawajaacha kumbukumbu ya utawala wa watoto wao kwenye siasa za kidemokrasia .
Mfano mzuri kwa Tanzania ni Mzee Mwinyi na Kikwete waliimarisha demokrasia kwa vitendo . Leo watoto wao wanaaminika na kupata nafasi za juu .
Hivi ni nani atampigia kura mtoto wa mbowe siku akitaka kuongoza chama wakati kuna historia ya udikteta ya baba yake kuwamaliza wenzake kwa fitina na kuwalengesha kwenye mikono ya dola .
Ukimsikiliza Mbowe hana hoja yoyote ya kwa nini ana ngangania kiti wakati amepoteza ushawishi kwa siasa za woga na maviziano ya woga aliyoyaomba mwenyewe ili asije akafungwa kwa ugaidi wake .
Mbowe na Serikali ya CCM hana tofauti na Osama Bin Laden na serikali ya Marekani ambayo ndiyo iliyokua inamfadhili na kumtumia kuwamaliza maadui zao.
Walipomuona wakamwita gaidi . Kwa hiyo Mbowe naye akitumika sana kuhujumu upinzani ili isishuke Dola na wanajua ndizo maana wakamshitaka kwa ugaidi waliokuwa wanaijua .Kuna Bomu liliwahi kurushwa kwenye mkutano wa Chadema kule Arusha . Uchunguzi wa polisi ulionyesha kuwe Chadema ndio waliokua wamelipua watu .
Kwa Haya ya Mbowe na Hotuba zake na jinsi anavyoegemea upande wa Serikali kuliko kwa mgombea wake aliyekua amemteua kugombea Urais ni wazi kuwa Lile bomu lilirushwa na genge la Mbowe kama gaidi mkuu na vyombo vya dola walikua wanajua ndio maana walisema limerushwa na Wanachadema wenyewe . Wakati huo Mbowe alikua Mwenyekiti. Hatukusikia akisema habari ya uchunguzi wa Scortland yard.
Huyu Mbowe ni mtu wa kuwa naye makini sana . Stahili yake kwa sasa ni kukataliwa kwenye kura maana kubaki na gaidi kwenye chama ni kuhatarisha maisha ya vijana wenye Moyo wa kupigania haki kwenye nchi hii.
Sura halisi ya Mbowe imeonekana.
Wanasema ni Mzee wa Busara lakini wanasahau kuwe Hata Dr.Samia ana busara sana lakini maamuzi yake ni hatari sana. Ndio kama yale ya kuwakata watu mikia . Lakini sio hivyo tu hata wale aliowateua kwenye vyombo vyake vya dola ni wale wale waliowashughulikia wapinzani kisawasawa . Lakini Mbowe wala hakushtuka kwa sababu anaona yeye hahusiki zaidi ya kufanya maigizo ya kumkamata na kumuweka ndani huku wenzake wakipotea au kujeruhiwa .
Haiwezekani matukio yote yaliyosababisha mauaji na watu kupigwa na kujeruhiwa yawe yametokana na kauli za Mbowe halafu cha ajabu anaambiwa kuwe ana busara kubwa na anachagua maneno ya kuongea .
Aliyetoa kauli ya kihaini na kuleta mtafaruku uliovuruga mwenendo mzima wa kisiasa ni huyo huyo Mbowe kwa kauli yake ya "Samia Must Go." Hii ni kauli iliyoleta taharuki kubwa saa ana lakini CCM na genge la Mbowe hawaoni kuwa huku kuropoka kulikua kunataka kuleta mapinduzi . Wao wanaangalia kuropoka kwa kuwataja mafisadi na kusema mafisadi hawastahili kupewa uongozi ndani na nje ya chama . Huyu Mzalendo eti hana busara wakati hakuwahi kuhamasisha watu wafanye vurugu kama Mbowe aliyehamasisha mauaji ya Aquiline kwa kauli za hotuba zisizo zingatia sheria za nchi.