Wewe nina uhakika hata genge la nyanya hujawahi miliki... Hivi Baresa na Mengi walianza lini biashara?Miaka 18 kwenye biashara umezeeka ,huwezi mbinu mpya waachie vijana..
Ni ngumu sana kumfundisha mbwa mzee mbinu mpya
Sent using Jamii Forums mobile app
Nina miaka 18 kwenye biashara katika kipindi chote hicho,Nimepitia milima na mabonde.” Yani changamoto” Kitu ambacho ni cha kawaida kwenye biashara yoyote.
Lakini leo nakiri kwamba, Awamu hii imeuwa juhudi za watu wengi kufikia malengo yao kibiashara, Biashara zimeyumba kabisa, Mauzo yameshuka kwa asilimia zaidi ya 70, huku mitaji mingi ya wajasiria mali ikiteketea.
Kinachoogopesha zaidi, Sioni juhudi zozote za makusudi kuokoa hali hii mbaya. Jamaa zangu wengi wameshindwa kulipia school fees,Wengine wameshindwa kulipia mapango ya frem,Wengine ndoa zao zimevunjika na wengine wamepata stroku.
Lakini tukiwasikiliza viongozi wetu wanasema tupo pazuri. Najiuliza pazuri wapi?
Mwanzoni nilijua labda baba anafanyia nyumba usafi, Cha kushangaza tunamaliza miaka tano hali imekuwa tete zaidi ya tulipo toka.
Kuna hitajika jitihada za ziada kwenye uchumi wetu tena kwa speed kubwa la sivyo tutazalisha taifa la wamachinga na wapiga vibomu. Maana soon kodi za pango na serekali hazitalupika tena.
Natamani hii biashara yangu nimpe bure Dr mpango aiendeshe kwa miezi tu ili ajue hali halisi sio kukaa ofisini huku tukimlipa mshahara mnono bila kusaidia uchumi wetu.
Dr. Mpango mweleze rais hali mtaani ni mbaya,Watu tunapiga kazi asubuhi mpaka jioni lakini tunatoka kapa kila siku.
Halafu nimegundua ukiwa na hali mbaya mfukoni na majukumu ndio yanabisha hodi kwa kasi kweli kweli.
Hivi ilani ya chama ndio ilinadiwa kutekeleza hali iwe ngumu hivi? Tukutane mwakani october tuelezane kwa vitendo.
Biashara karibu zote tu, mi nipo kkoo mtu unawahi unafungua duka saa moja asubuhi, mpaka inafika saa nne hata mteja kuja angalau kuuliza bei tu hamna!Unafanya biashara gani? Ni nini unachoona tofauti na wakati mwingine? eg. kodi imekuwa kubwa, wateja wamepungua etc..
Achana nae mpuuzi huyo, hata ma bank teller wenyewe wanachezea simu tu.Muoneni huyu bank teller!!!
Tafadhali tusitafutiane BAN zisizokuwa za lazima,tafwadhali sana!
Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
Mtoa mada hajalalamika kulipa kodi!ukizoea kunyonga,kuchinja huwezi
Sasa ni kulipa kodi tu,kwa kua ulizoea kulipalaki tano kwa mwaka,lazima hali uone ngumu
Sio kama kubet sima kubeti ndio biashara wawamu hii inayolipa.Biashara ya awamu hii ni kama mchezo wa kubeti
pole sana!Mm nmetoka leo kupoteza kibarua changu rasmi biashara imefungwa. Wala sio kwasababu ya maamuzi ya bosi. Hapana biashara haiko vzur hata ww mfanyakazi unaona kabisa kuwa ikiendelea hivi bas kibarua kinaota nyasi..
Hatimae siku imefika nimerud mtaani.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna kitu kimoja ambacho wanaojiita wafanyabiashara hasa wa Dar ambacho hawakioni. Utitiri wa biashara za aina moja kwenye kila sehemu ya Dar nayo unachangia. Huwezi kuwa na jiji ambalo kila mtaa nyumba za barabarani wamejenga vibanda vidogo vidogo vinavyoita fremu na kwenye kila frem bidhaa ni za aina moja halafu utegemee biashara isifikie kwenye ''turning point'' siku moja. Jamani kama hiyo Kariakoo unayosema kila nyumba imegezwa ya biashara. Na mbaya zaidi nyumba moja imeganywa ''vichochoro'' vidogo vidogo vingi vinavyoitwa frem. Na kuweka chumvi kwenye kidonda bidhaa karibu zinafanana fanana. Hata Magufuli asingeingia madarakani nakuhakikishia hii hali lazima ingetokea tu.Biashara karibu zote tu, mi nipo kkoo mtu unawahi unafungua duka saa moja asubuhi, mpaka inafika saa nne hata mteja kuja angalau kuuliza bei tu hamna!
kwa kifupi uwezo wa watu kununua bidhaa umeshuka kwa kiasi kikubwa sana, tunasinzia tu madukani.
007 james Bond
Hata plate number kwa mara ya kwanza zimechelewa kubadilika, 2015 niliingiza gari nikapata number DCY mwaka wa 5 huu bado tupo kwenye D haijawahi tokea.Ninachoshangaa ni kwamba plate no za magari zimefika DQ....
Mkuu unatushauri nini tunaotaka anzisha biashara kwa sasa?
Ije mara ngapi wakati yashatimiaZimbabwe Leo hii Watu zaidi ya milion 5 wanahitania msaada kutokana na uchumi wa taifa lao kuwa duni,lkn Cha kushangaza viongozi wa Zimbabwe wamezidi muwa mabilionea wa mutupwa
Roma mkatolika Zimbabwe inakuja
Sent using Jamii Forums mobile app