Kwa miaka 18 sijawahi kushudia ugumu wa biashara kama awamu hii ya Tano

Kwa miaka 18 sijawahi kushudia ugumu wa biashara kama awamu hii ya Tano

Nina miaka 18 kwenye biashara katika kipindi chote hicho,Nimepitia milima na mabonde.” Yani changamoto” Kitu ambacho ni cha kawaida kwenye biashara yoyote.

Lakini leo nakiri kwamba, Awamu hii imeuwa juhudi za watu wengi kufikia malengo yao kibiashara, Biashara zimeyumba kabisa, Mauzo yameshuka kwa asilimia zaidi ya 70, huku mitaji mingi ya wajasiria mali ikiteketea.

Kinachoogopesha zaidi, Sioni juhudi zozote za makusudi kuokoa hali hii mbaya. Jamaa zangu wengi wameshindwa kulipia school fees,Wengine wameshindwa kulipia mapango ya frem,Wengine ndoa zao zimevunjika na wengine wamepata stroku.
Lakini tukiwasikiliza viongozi wetu wanasema tupo pazuri. Najiuliza pazuri wapi?

Mwanzoni nilijua labda baba anafanyia nyumba usafi, Cha kushangaza tunamaliza miaka tano hali imekuwa tete zaidi ya tulipo toka.

Kuna hitajika jitihada za ziada kwenye uchumi wetu tena kwa speed kubwa la sivyo tutazalisha taifa la wamachinga na wapiga vibomu. Maana soon kodi za pango na serekali hazitalupika tena.

Natamani hii biashara yangu nimpe bure Dr mpango aiendeshe kwa miezi tu ili ajue hali halisi sio kukaa ofisini huku tukimlipa mshahara mnono bila kusaidia uchumi wetu.

Dr. Mpango mweleze rais hali mtaani ni mbaya,Watu tunapiga kazi asubuhi mpaka jioni lakini tunatoka kapa kila siku.

Halafu nimegundua ukiwa na hali mbaya mfukoni na majukumu ndio yanabisha hodi kwa kasi kweli kweli.

Hivi ilani ya chama ndio ilinadiwa kutekeleza hali iwe ngumu hivi? Tukutane mwakani october tuelezane kwa vitendo.

Mwanangu pambana na hali yako. Siye mbele kwa mbele.
Kipindi hiki nimeweza kununua ndinga, kujenga house (siyo nyumba, namaanisha mjengo).
Nimepanda ndege
Nimefika uropa.

Hahahaha, awamu ya 5 ni zamu yetuuuuuuu
 
Unafanya biashara gani? Ni nini unachoona tofauti na wakati mwingine? eg. kodi imekuwa kubwa, wateja wamepungua etc..
Biashara karibu zote tu, mi nipo kkoo mtu unawahi unafungua duka saa moja asubuhi, mpaka inafika saa nne hata mteja kuja angalau kuuliza bei tu hamna!
kwa kifupi uwezo wa watu kununua bidhaa umeshuka kwa kiasi kikubwa sana, tunasinzia tu madukani.

007 james Bond
 
Muoneni huyu bank teller!!!

Tafadhali tusitafutiane BAN zisizokuwa za lazima,tafwadhali sana!

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
Achana nae mpuuzi huyo, hata ma bank teller wenyewe wanachezea simu tu.
Atakuwa anakaa kwa shemeji! ndio akili zao zinakuwaga hivyo.

007 james Bond
 
Mm nmetoka leo kupoteza kibarua changu rasmi biashara imefungwa. Wala sio kwasababu ya maamuzi ya bosi. Hapana biashara haiko vzur hata ww mfanyakazi unaona kabisa kuwa ikiendelea hivi bas kibarua kinaota nyasi..

Hatimae siku imefika nimerud mtaani.

Sent using Jamii Forums mobile app
pole sana!

007 james Bond
 
Mkuu unatushauri nini tunaotaka anzisha biashara kwa sasa?
 
Biashara karibu zote tu, mi nipo kkoo mtu unawahi unafungua duka saa moja asubuhi, mpaka inafika saa nne hata mteja kuja angalau kuuliza bei tu hamna!
kwa kifupi uwezo wa watu kununua bidhaa umeshuka kwa kiasi kikubwa sana, tunasinzia tu madukani.

007 james Bond
Kuna kitu kimoja ambacho wanaojiita wafanyabiashara hasa wa Dar ambacho hawakioni. Utitiri wa biashara za aina moja kwenye kila sehemu ya Dar nayo unachangia. Huwezi kuwa na jiji ambalo kila mtaa nyumba za barabarani wamejenga vibanda vidogo vidogo vinavyoita fremu na kwenye kila frem bidhaa ni za aina moja halafu utegemee biashara isifikie kwenye ''turning point'' siku moja. Jamani kama hiyo Kariakoo unayosema kila nyumba imegezwa ya biashara. Na mbaya zaidi nyumba moja imeganywa ''vichochoro'' vidogo vidogo vingi vinavyoitwa frem. Na kuweka chumvi kwenye kidonda bidhaa karibu zinafanana fanana. Hata Magufuli asingeingia madarakani nakuhakikishia hii hali lazima ingetokea tu.
 
Tatizo kubwa kuliko yote linayoigharimu Tanzania ni kwenye maamuzi yani mtu anaeamua hatma ya wafanyabiashara sio mfanyabiashara mfano Kenya wao viongozi wao wengi ni wafanyabiashara hivyo wanaweka mazingira mazuri na marahisi ili biashara zao ziweze kushamiri vizuri lakini huku unamkuta mtu amekaa ofisini na tai shingoni anaamka anasema kuanzia kesho tupandishe tozo fulani, ongeza tozo hii serikali itapata mapato yani sehemu kubwa yenye tatizo ni hio, awamu iliopita ilikua inaunafuu sababu yule jamaa alietoka alikua na elements na michakato ya kibiashara sasa hivi yupo mtu katoka bush huko lakini anaamua mambo mpaka unashangaa..
 
Mkuu unatushauri nini tunaotaka anzisha biashara kwa sasa?

Usithubutu mkuu,Afadhali huyo mtaji ukaweke fixed account then ubangaize mpaka siku mambo yakibadilika ndio ufikirie kuhusu biashara ya kununua na kuuza. Ukianzisha biashara sasa nakupa miezi 3 tu mtaji utakuwa umeteketea.Hali ni mbaya mno, Nguvu ya manunuzi imeshuka mpaka kwenye vyakula. Bajeti za nyumbani hazipangiki,Na ukipanga bajeti nyumbani lazima nyama na samaki iwe kwa wiki mara moja. Hali ni mbaya mno!
 
Nilishafunga biashara zangu mbili ya printing na stationery na vifaa vya umeme na solar baada ya kuona biashara mauzo yameshuka kwa 50% unajikuta kila wakati unatakiwa kuiboost kwa kuongeza mtaji ukiangalia mikopo kibao.

Nimengia kwenye kilimo na mazao huku sikutani na TRA wala kodi ya pango wala kumlipa mfanyakazi baada ya miaka 2 mungu akitupa uhai basi huko mjini nitakuja kuulizia ni gari gani mpya inatamba mjini nimunue.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwakweli ukifanikiwa kutoboa awamu hii,hutakaa ufilisike tena kibiashara.Mambo yamekua hovyo biashara haipo kabsa,Wengi wamepoteza mitaji yao.Wafanyabiashara tuna hali ngumu sana[emoji22]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom