Kwa miaka 18 sijawahi kushudia ugumu wa biashara kama awamu hii ya Tano

Kwa miaka 18 sijawahi kushudia ugumu wa biashara kama awamu hii ya Tano

Miaka 18 kwenye biashara umezeeka ,huwezi mbinu mpya waachie vijana..

Ni ngumu sana kumfundisha mbwa mzee mbinu mpya

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa kuwa nyie mmetoka Kolomije juzi, mnaona kila mtu hapa mjini kaanza gemu juzi. Kwani Bakhresa ana miaka mingapi kwenye biashara? Au mnazungumzia chinga wauza maji ya Kondoro?
 
Nimekuuliza mana naona umetanguliza tumbo wazi mbele kwa kuanza kupondea halafu huna chochote ulichoshauri katikati ya malalamiko yako sababu unakuwa kama mpiga zumari.
Ushauri gani wakati watu walikimbilia ''fuata mkumbo'' bila kujiuliza. Hakuna ushauri ila hasara ndiyo itawapa akili.
 
Lakini hardwares zipo busy, magari mapya tele mitaani, bar zinajaa pomoni

Wewe kama ilikuwa hulipi kodi kihalali ndio inakula kwako au kama biashara au wateja wako wengi wana linkage na zile sector zilizokua za kifisadi

Kuna biashara iliyokua maarufu nchi hii kama madawa ya kulevya? Viroba? Meno ya tembo? Wizi Bandarini? Wizi wa halmashauri? Sasa hayo mabilioni kwenye hayo maeneo ndio yalikua yanazagaa mitaani hovyo bila uchungu wala jasho, sasa hayapo tena lazima muone maisha hayaendi.
 
Lakini hardwares zipo busy, magari mapya tele mitaani, bar zinajaa pomoni

Wewe kama ilikuwa hulipi kodi kihalali ndio inakula kwako au kama biashara au wateja wako wengi wana linkage na zile sector zilizokua za kifisadi

Kuna biashara iliyokua maarufu nchi hii kama madawa ya kulevya? Viroba? Meno ya tembo? Wizi Bandarini? Wizi wa halmashauri? Sasa hayo mabilioni kwenye hayo maeneo ndio yalikua yanazagaa mitaani hovyo bila uchungu wala jasho, sasa hayapo tena lazima muone maisha hayaendi.

Kuna mdau alizungumzia kuhusu black market. Akatolea mfano nchi ya Mexico
Kama ulimwelewa ungeandika kitu ulichoandika
 
Mada za namna hii ndizo ambazo zinafikirisha na kuleta mijadala ya nguvu...lakini nikwambie kitu ndugu yangu ...hali ya sasa ndiyo hali halisi...kwa miaka mingi watanzania tulikuwa hatuishi maisha halisi....haya ndiyo maisha yenyewe kiuchumi...kwamiaka mingi tulikuwa tunaishi maisha ya wizi wizi...fedha chafu za rushwa bandarini...wizi wa mafuta yasiyolipiwa kodi..tenda za ujanja serikalini...maofisi mengi ya brief case...wizi fedha za umma...kutofanya kaziserikalini na kufanyia mikutano kwenye mahoteli baadala ya ofisini...wizi wa mali za umma...sasa serikali hii imejaribu kuziba mianya hiyo...hakuna tena fedha chafu au za dezo...yaani fedha za aina hiyo zimepungua mno..sasa tunaishi maisha halali...tunatakiwa tufannye kazi...baada ya miaka kumi hivi hali itatengemaa...labda...madalali poleni sana yaani madalali wa nyumba, mashamba na kadhalika...
Yaan nikisikia point zenu nawaonea huruma sana maana hamuijui ya kesho. Biashara nyingi hasa za maduka zinakufa tokana na sera mbaya. Mfano ile kuruhusu machinga mpaka milangon imevunja mitaji ya watu waliokuwa wananunua na kuuza kwenye frame zao.
Zuio la mazao kusafirishwa pasipokuwa na sabab za msingi, hapa kuna korosho, kahawa, mahindi na na mengine mengi. Baada ya kuzia haya mazao ambayo yalikuwa yanaingiza pesa za kigen hali imeendelea kuwa mbaya.
Kuongeza kodi kadha wa kadha. Mfano kod ya lesen ya kusafirisha samaki wazima kama kaa toka 280k mpaka almost usd 2500 kwa kila aina ya samaki. Hii imepelekea wafanyabiashara wengi kuachana na hiz biashara na badala yake kuachisha watu kazia ambao ndo walikuwa ndo wanunuz wakubwa wa nguo,chakula, kondom na hata dada zako.
Kesi nyingi za uhujumu uchumi zisizo na maana zimewatisha wawekezaji wengi na wale wachache waliopata nafasi mwanzoni wa kutoa mitaji yao, wamehamia nchi nyingine kama zambia,msumbij, kongo na hawa wote walikuwa wanaajiri watu ambao ndo walikuwa wanunuz wakubwa.
 
Wakati Magu anaingia ndio nimeanza biashara ninayoifanya nilikuwa na kafremu kamoja. Sasa hivi nimechukua fremu nne, nimejenga nyumba moja, ya pili namalizia, nimenunua gari ya pili January. December nimeenda vacation wiki moja Dubai. Labda inawezekana ingekuwa awamu iliopita ningepata mafanikio zaidi ya hayo.

Ndani ya miaka minne tu! Unafaidika nini kudanganya watu usiowajua?
 
Back
Top Bottom