Kwa miaka 18 sijawahi kushudia ugumu wa biashara kama awamu hii ya Tano

Kwa miaka 18 sijawahi kushudia ugumu wa biashara kama awamu hii ya Tano

Nina miaka 18 kwenye biashara katika kipindi chote hicho,Nimepitia milima na mabonde.” Yani changamoto” Kitu ambacho ni cha kawaida kwenye biashara yoyote.

Lakini leo nakiri kwamba, Awamu hii imeuwa juhudi za watu wengi kufikia malengo yao kibiashara, Biashara zimeyumba kabisa, Mauzo yameshuka kwa asilimia zaidi ya 70, huku mitaji mingi ya wajasiria mali ikiteketea.

Kinachoogopesha zaidi, Sioni juhudi zozote za makusudi kuokoa hali hii mbaya. Jamaa zangu wengi wameshindwa kulipia school fees,Wengine wameshindwa kulipia mapango ya frem,Wengine ndoa zao zimevunjika na wengine wamepata stroku.
Lakini tukiwasikiliza viongozi wetu wanasema tupo pazuri. Najiuliza pazuri wapi?

Mwanzoni nilijua labda baba anafanyia nyumba usafi, Cha kushangaza tunamaliza miaka tano hali imekuwa tete zaidi ya tulipo toka.

Kuna hitajika jitihada za ziada kwenye uchumi wetu tena kwa speed kubwa la sivyo tutazalisha taifa la wamachinga na wapiga vibomu. Maana soon kodi za pango na serekali hazitalupika tena.

Natamani hii biashara yangu nimpe bure Dr mpango aiendeshe kwa miezi tu ili ajue hali halisi sio kukaa ofisini huku tukimlipa mshahara mnono bila kusaidia uchumi wetu.

Dr. Mpango mweleze rais hali mtaani ni mbaya,Watu tunapiga kazi asubuhi mpaka jioni lakini tunatoka kapa kila siku.

Halafu nimegundua ukiwa na hali mbaya mfukoni na majukumu ndio yanabisha hodi kwa kasi kweli kweli.

Hivi ilani ya chama ndio ilinadiwa kutekeleza hali iwe ngumu hivi? Tukutane mwakani october tuelezane kwa vitendo.
[emoji1318]
HII NCHI NI YETU SOTE
NA
MAENDELEO HAYANA CHAMA!!!!
[emoji1318][emoji1318][emoji1318]

"ILA MAISHA LAZIMA YAENDELEE."
 
Na hivi jua limechachamaa na mvua imegoma.kitaeleweka tu maana zaidi ya 90 % ya watanzania wanategemea kilimo kuendesha maisha yao. Itajulikana tu .
 
Mada za namna hii ndizo ambazo zinafikirisha na kuleta mijadala ya nguvu...lakini nikwambie kitu ndugu yangu ...hali ya sasa ndiyo hali halisi...kwa miaka mingi watanzania tulikuwa hatuishi maisha halisi....haya ndiyo maisha yenyewe kiuchumi...kwamiaka mingi tulikuwa tunaishi maisha ya wizi wizi...fedha chafu za rushwa bandarini...wizi wa mafuta yasiyolipiwa kodi..tenda za ujanja serikalini...maofisi mengi ya brief case...wizi fedha za umma...kutofanya kaziserikalini na kufanyia mikutano kwenye mahoteli baadala ya ofisini...wizi wa mali za umma...sasa serikali hii imejaribu kuziba mianya hiyo...hakuna tena fedha chafu au za dezo...yaani fedha za aina hiyo zimepungua mno..sasa tunaishi maisha halali...tunatakiwa tufannye kazi...baada ya miaka kumi hivi hali itatengemaa...labda...madalali poleni sana yaani madalali wa nyumba, mashamba na kadhalika...
Hebu eleza vizuri kwanza!maisha halisi ya kuwa na hali mgumu hata Kwa mkulima aliyelima mahindi,mbaazi,korosho n.k nae alikuwa anaiiba?acheni kukariri Kwa kukubali. Et wanaolalamika wapiga dili!mkulima wa korosho ,mahindi ,mbaazi nao wapigadili?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Weka facts sio unaleta hadith zabkusadikika tuuu maelezo mengi hakuna facts.
 
Hali imekuwa mbaya sana,kuna watu wanakufa kutokana na hali ya maisha huku mtaani,wastaafu hawajalipwa hata cent moja,biashara zimekufa,watumishi hawajapandishwa madaraja wala kulipwa mapunjo,ndoa zimefurugika na watu wameacha kuwasaidia ndugu zao

Wenye maisha mazuri hivi sasa ni Paulo Matter-core na Stone
Sina uzalendo tena kwa Taifa langu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom