Kwa miaka 20, sijaongezeka uzito hata kilo moja wala sijazeeka

Mdukuzii

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2022
Posts
2,552
Reaction score
6,422
Kwa miaka 20 kilo zangu ni zilezile sijaota mvi au kuzeeka, nilizaliwa nao ni wazee mimi niko vilevile, vibinti vya miaka 20 vinaniambia mambo wakati ninesoma na mama zao.

Hii hali inakera sipati heshima yangu, kuna mzee jirani yangu hajui jina langu huwa ananiita we kijana...sipendi.
Kwenye kupeleka moto napeleka kama enzi niko teenager

Je mimi ni mzima au nilishakufa
 
Jiangalie vizuri inawezekana hizi post unatuma ukiwa jehanamu tayari...
 
Namba haijawahi kudanganya kamwe!

Kioo kitakudanganya vyovyote vile ukijitazamapo kwa u-handsome/u-beautiful, lakini kiukweli nguvu za mwilini mwako ulizokuwa nazo miaka mi5 au 10 iliyopita haziwezi tena kuwa katika kiwango/uwezo ule ule.

Imeisha hiyo............
 
Dah kumbe tupo wengi
 
Kama unaimani sana na Mungu basi ujana wako umerejeshwa kama tai...

Ila kama ni imani haba unatumiwa na mshetani ili ubakie kijana...
 
Nadharia yangu ni kwamba;

Matumizi yako ya muda-michakato ni madogo.

Muda-michakato: Ni idadi ya mambomambo yote unayoyafanya kuishi mfano kula, kutembea kufanya kazi labda yapo polepole, yaani unafanya machache ndiyo maana muda wako unaonekana kibinafsi kwenda slow - relativity.

Mfano wa extreme case ni kobe na nzi, kobe na nzi wana umri mmoja wa kuishi katika kipimo cha muda-mchakato.
Ila nzi anazaliwa anakula harakaharaka, anakimbiakimbia hapa na pale anapevuka na kuzaa fasta hadi muda-michakato wake unaisha fasta anakufa. Lakini kobe anaenenda polepolee kila mchakato hadi kuja kuimaliza michakato yake ndio muda-mchakato unaisha anakufa naye.

So kwa binadamu wawili tulio na utashi muda unaenda tofautitofauti sana, mfano alovuta bhangi na asiyevuta sasa uje umlinganishe na aliyelewa mda wao ni tofauti.

Kwa kuwa una kilo zilezile inaonesha mchakato-ulaji wako inapunguza muda....... aah maelezo yanakuwa mengi ila tafiti zinaonesha uhusiano wa mojakwamoja katinya calories anazomeza kiumbe na umri wake. Kuna wadudu wanakula mara mbili ya mwili wao hawanaga maisha marefu, na panya waliopunguziwa calories waliishi zaidi

Labda inaaplai kwetu sijui, bado ni nadharia.
 
Kwanza mkuu ulipotelea wapi
 
Unautamani uzee ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…