Kwa miaka 20, sijaongezeka uzito hata kilo moja wala sijazeeka

Hii naona ina aplai kwetu na viumbe wote. karibu viumbe wote wanaoishi maisha marefu hawali sana na hawatembei tembei sana au haraka haraka mfano Greenland sharks na kobe.

Angalia hata watoto wanaokula sana wakiwa wadogo wanakuwa haraka na kuzeeka haraka.
 
2015 nilienda kuchangia damu kupima uzito nikakuta 74
2019 nikapima nikakuta 74
2022 mwezi 4 nikapima tena nikakuta na 73.4
Nadhani nijambo la kawaida
 
Exactly, maisha yakienda kasi yanaenda kasi kwelikweli. Yas greenland sharks nawakumbuka niliwasomaga eti kasi yao kuogelea hadi binadamu anawashinda, wameamua kulaga hadi mizoga na waliolala[edited baada ya kupitia tena] maisha yanasonga hawana shida yaani

Na hakuna ambaye anajipunja wala, ile jumla ya uzoefu na raha/shida ni sawa sema mmoja amechagua kuzifaidi kwa karibukaribu mwingine ameziachanisha mbalimbali ila wote wanapata na kufurahia stahili yao yote.
 
Sasa huu uzi bila picha unakua na ukakasi kidogo.

Inabidi watu tuone tujiridhishe kwamba kweli bado unamuonekano wa kijana mbichi.

Unaweza kuwa uko mkavu vilevile lakini uzee haujifichi. Kumbuka muonekano wakizee hauonyeshwi Kwa mvi pekee.
 
sahihi.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Utakuwa umeshakufa.....Jokes
 
Dah hapa umenifundisha kitu kweli.ulaji wangu sio mzuri sana pia nina ideas nyingi ila utekelezaji ni slow sana,labda Mungu anasubiri nitimize idea zangu ndio nizeeke nife.niliwahi kuitwa kucheza filamu wakahitaji mtu mwenye umri kama wangu,kwenda director akanikataa akasema naonekana mdogo
 
Hongera sana mkuu. Hata mm watoto wangu (kiumri) huwa wananiona ni kijana mwenzao. Binafsi huwa sipendi hali hiyo, japo uzee nao sio mzuri sana.

Hata nikiwa njiani na mke wangu huwa wanamsalimia mke wangu, "shikamoo mama" kwangu wananiambia "za saizi kaka". It is boredom, but ...




YESU KRISTO NI BWANA
 

Huyo director nae haeleweki. Alitakiwa ajikite kwenye muonekano sio umri. Kuna watu Wana umri mdogo wanaonekana watu wazima kuliko umri wao. Wengine Wana umri Mkubwa lakini ndio kama vijana. Kama alitakiwa ajikite kwenye muonekano, filamu watu wanaona hawahangaiki na umri.
 
Hiyo ni moja kati ya mibaraka ya kuifurahia.

Mi bado nipo dilema;

Je nitafute mke mwenye muonekano wa ukubwa ili watu wajue mi mkubwa automatiki kwamba 'unamjua mke wake? kale kajamaa ni kakubwa basi tu'

AU nioe mdogo zaidi ili asinipite nikapata kadhia unayokumbana nayo yaani sijajua asee
 
Ndiyo exactly director alichofanya, aliangalia muonekano na sio umri
 
Ndiyo exactly director alichofanya, aliangalia muonekano na sio umri

Ndio maana nikasema, tokea awali, alitakiwa aweke kigezo Cha muonekano, hata usingehangaika kwenda. Alivyotaja umri flani mwanzoni ukaenda Kwa kujua atazingatia umri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…