Kwa miaka 5 na miezi kadhaa, yaani kuanzia 2015 hadi March 2021 Magufuli amekopa kiasi cha Trillioni 36, kwa wastani wa Trillioni 7 kwa mwaka.
Magufuli amefariki March 2021 Deni la Taifa liko Trillioni 72. Kwa muda wa miezi 9, yaani kuanzia March 2021 hadi December 2021 deni la Taifa ni Trillioni 82, kwa maana kwamba kwa miezi 9 mama amekopa Trilioni 10.
Tukienda kwa kasi hii ya mikopo, miaka 4 ijayo mama atakopa Trillioni zaidi ya 50 na kufanya deni la Taifa kufikia Trilioni 120 ama zaidi mwaka 2025.
Ndugai yuko sahihi, spidi ya kukopa ni kubwa sana. Mama hataki kuangalia vyanzo vipya vya kodi, yeye anakimbilia the easy way out, kukopa, kukopa na kukopa.
Hii nchi miaka 60 ya uhuru tunakopa kujenga madarasa, kujenga vyoo kweli? Hata hilo la ujenzi wa vyoo vya shule tunahitaji kukopa? Tukope kufanya vitu vya msingi.
Kuna watu wasema mama ameleta uwazi wa matumizi ya mikopo sio kama Magufuli, naomba tuulizane, kwenye hizo Trillioni 10, tumetangaziwa matumizi ama mgawanyo Trillioni ngapi? Si hizi 1.5 za covid tu za ujenzi wa madarasa? Nyingine 8.5 tunajua zimetumika wapi?
View attachment 2063295