Kwa Milioni 30, UTT amis na nyumba ya kupangisha kipi bora?

Uko sahihi,akijenga nyumba asitegemee kupata hela kwa wakati labda ajenge kwa ajili ya kulala yeye na watoto wake.
 
Vipi hiyo uwekezaji wa UTT kwamba unataka kusema serikali hawana access nayo?yaani serikali wakihitaji kukopa huko itashindikana?
 
Milioni 30 utajenga nyumba ambayo utakuwa unapata si zaidi ya 250,000 kwa mwezi.

Itachukua miaka 10 ku breakeven hiyo milioni 30 yako. Ila thamani ya eneo pia itakuwa imeongezeka.
 
Uko sahihi,akijenga nyumba asitegemee kupata hela kwa wakati labda ajenge kwa ajili ya kulala yeye na watoto wake.
Ushauri wangu wa dhati.
Chukua iyo 30m ununue government bonds za 20 or 25 years. Utapata between 15.5 to 16% annual interest ambayo ulipwa kila miezi 6. Yaani hii ni clean money no longo longo.
Ukishapata iyo bond ombea mkopo ambao unawezapata up to 80% ya thamani ya bonds zako. Ukiwa na bonds banks wanatoa mkopo chap yaani no many questions. Mapato yako ya bonds ndio yanaenda kulipa mkopo. No stress za marejesho. Na ukimaliza mkopo 30m zako zipo palepale na utakula faida.
Then ukipata iyo cash jenga nyumba upangishe hapa utapata Mapato kila mwezi.
Yaani in short iyo 30m inaweza kukuzalishia cash na nyumba juu na ni guarantee utaipata baada ya miaka 20 au 25 kulingana na utakavyochagua. Na hata mambo yakikuendea vibaya ukaitaka hela yako kabla ya maturity unaweiza iuza kwenye secondary markert tena if you are lucky with interest.
Bonds unanunua kupitia kwa ma agent kama crdb Bank etc, wapo wengine wengi tu but make sure they are genuine.
Hope umeelewa.. Fene
 

Hii ina utofauti gani na UTT AMIS? (kiusalama wa pesa za mteja).

Ufafanuzi tafadhari.

-Kaveli-
 
Nyumba ya kupanga ya nn jenga lodge hata ya vyumba 5 tu
 
Ndugu unaongelea Kerege katika kitongoji gani kati ya hivi? Kitonga, Kwa Manofu, Amani, Nyakahamba, Matumbini, Kwakiwete au Kibemela?
 
Reactions: Tsh
Nipo hapa niendelee kuokota madini
 
Ila basi Tu tumetofautiana akili ila 30M ukiwa na biashara Una uhakika hata 500k daily profit...hata ukipata 1% bado ni faida kuliko utt unapata uzoefu
Sasa sijui ulipataje hiyo 30M
 
Ila basi Tu tumetofautiana akili ila 30M ukiwa na biashara Una uhakika at minimum kupata at 3% daily profit ambayo ni kama 900k daily...
Sasa sijui ulipataje hiyo 30M
Mzee πŸ˜‚πŸ˜‚
3% daily? Biashara gani hio?
 
Ningepeleka UTT hiyo Mil30, then naenda kukopa kupitia hiyo investment ya UTT ningepata kitu kama Mil 21 hapo sasa ndio naanzisha biashara au kilimo ambapo faida itakayopatikana ndio itakayokuja kujenga
 
Ningepeleka UTT hiyo Mil30, then naenda kukopa kupitia hiyo investment ya UTT ningepata kitu kama Mil 21 hapo sasa ndio naanzisha biashara au kilimo ambapo faida itakayopatikana ndio itakayokuja kujenga

Ukikopa 21m riba yake ikoje? Faida ya UTT ikoje.

Ukitoa FAIDA YA UTT toa Riba ya bank unabakiwa na nini?
 
Ndugu unaongelea Kerege katika kitongoji gani kati ya hivi? Kitonga, Kwa Manofu, Amani, Nyakahamba, Matumbini, Kwakiwete au Kibemela?
Boss, hii mada muda kama umepita hivi, nilitoa mfano tu.
 
Mil30 kilimo, vipuri vya magar!? Utaua watu na kihalusi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…