Kwa miongo ulioishi Duniani umejifunza nini?

yapo mengi ila machache ni haya:
1: Tulianza harakati za kufa, mara tu baada ya kuzaliwa.
2: Ukijiona unaweza, kuna mafundi zaidi yako.
3: utafahamika na watu kutokana juhudi zako au maarifa na kipaji chako.
4😀unia ni manukato yanayosahaulisha kifo.
5:kila rafiki wa kweli, anajifanya rafiki wa mafanikio yako.
6:Asilimia kubwa mzazi, wako akikutakia jema huwa ana maanisha kweli.
7:kama hautaki maadui, kaishi sayari ya peke yako.
8:misibani siku hizi, watu wanaenda kuonesha hali za vipato vyao na kuonekana.
9:Ni ngumu kurudisha maadili ya kizamani kwa njia za kisasa.
10:kama unapendwa jiulize, ni kwanini upendo hukamilika kwa kupendana.
 
Ccm ni mashetani
 
duna noma
 
"I have observed something else under the sun. The fastest runner doesn’t always win the race, and the strongest warrior doesn’t always win the battle. The wise sometimes go hungry, and the skillful are not necessarily wealthy. And those who are educated don’t always lead successful lives. It is all decided by chance, by being in the right place at the right time."

ecc.9.11.NLT
 
Muda ndiyo jibu la kila kitu.

Hali uliyonayo sasa ni suala la muda.

Kuna kipindi hata hutakuwa unafikiria kama uliipitia shida au raha unayoipitia muda huu.
 
Bahati ndio kila kitu Duniani,kuna watu wanazaliwa na bahati ya kuwa na akili nyingi,wengine kuzaliwa na bahati ya kuzaliwa kwa matajiri,bahati ya kuja kupata vyeo vikubwa,bahati ya kufanikiwa kibiashara,bahati ya kupata mahusiano mazuri,bahati ya kuwa,bahati ya kuwa na afya njema na bahati ya kuwa familia nzuri.

Kila kitu ni Bahati.
 
Mimi hili nimejifunza tofauti.

Nimejifunza kama unataka mafanikio fanya kazi. Kazi inaanzia unavyofikiri.

Kwa miongo kadhaa sijafanikiwa na aliyefanikiwa mvivu(lazy).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…