Kwa mjazano huu wa ndugu, sahau kabisa kuitwa tajiri

Ukiona wamekuwa wengi kwako hawana kazi anzisha Banda la kuku na Mbuzi mmoja asubuhi anakusanya mayai ya kuku mwingine anashinda anakwenda kuchunga Mbuzi.
Unaanzisha na bustani ya mbogamboga mmoja kazi yake kumwagilia bustani na kusupply mchicha na nyanya chungu kwa majirani.

Unapata labour force bila kulipia win win situation.

Watu wenye muda usio na matumizi huwa hawafukuzwi unatafuta tu matumizi ya muda wao.
 
Ni wingi wa watu na wafuasi
 
Utajiri sio mpaka uwe na Mali zinzoonekana hata kukaa na ndugu zako wanakula na kunywa huo pia ni utajiri wa roho mkuu .

Maisha mnayachulia serious mpaka yanakosa ladha.
Hii ishu anaepitia anko mmoja hivi kiukwel ukimtembelea unamuonea huruma,
Chakushangaza Kuna stori kanipa Kua mtu wake wakaribu kajenga kwao kimya kimya nakapewa taarifa nyumba ishaisha kisa tu Kua alikua aboreshi nyumba yao hivyo akaonekana nimbishi au mgumu kufanya maboreshe..
Kasahau kama ndugu wauoande wake wamejazana kwake
 
Maisha yenu yanashangaza sana
Kwanini hamtaki kubadilika?
Mtakuwa hivyo mpaka lini?
Hii tabia hamuezi kuacha ni kama dhulma, wizi na utapeli na Rushwa

Hambadiliki kwa sababu mmeufanya ndio mfumo wenu wa maisha

Jiulize mtu anakuwa na jeuri ya kuhamia kabisa kwako bila ridhaa yako, na wewe upo kimya kabisa

Hayo ndio maisha mliochagua lazima muwafunze watoto wenu kujitegemea.

Haya mambo huwezi kuyakuta kwa wengine kwani wanaanza kuwalea watoto wao tangu wadogo na kujua chao

Kuwafukuza huwezi kwa sababu ndio maisha yenu hayo
 
Ushauri mzuri
 
Mtoa mada unataka kuwa richest or wealthiest ?

Ikiwa unataka kuwa richest waweza kukaa peke yako na ukawakataa ndugu kwakuwa being richest ni kuwa na hela nyingi kuliko mali Ila kuwa wealthiest ni kuwa na Mali nyingi kuliko hela (Currency)

Mali nyingi zinaambatana na kukaa na watu ambao unaweza kuwageuza Kama rasilimali Kama kuwaweka katika mashamba , kusimamia buashara n.k
 
Atumie hayo anayoyaona kua ni matatizo kwake kua Fursa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…