Kwa mjazano huu wa ndugu, sahau kabisa kuitwa tajiri

Kwa mjazano huu wa ndugu, sahau kabisa kuitwa tajiri

Umefanikiwa kujijengea Nyumba Yako nakigari kidogo tu, unaamua sasa uanze kujiwekeza zaidi kwenye BIASHARA namambo mengine kipato kikue,

Upande wapili ndugu wa upande wako naukweni wanaanza kujazana ndani yanyumba Yako, nibora wakutembelee nakutoka lakini wanageuza makazi Yani mpaka binadamu wako😂 nae anakomaa hapo hapo..

Hao wote hawana kazi inabid uwalishe nakuwavesha sasa huo utajiri utaupata kweli sio kuishia kupata hela yakula tu

Uliwezaje epuka hali hii, nami nimshauri uncle wangu hapa..
Kuwa Mjanja......kuwa kama Mhindi, acha kulalamika.

Mhindi unakuta Mwenye hela n mmoja lajini anaishi na Watu zaidi ya 20 nyumbani kwake. Hadi watoto wa Binamu.

Anafanikiwa vipi?

Mostly ni vijana wametoka familia duni lkn wana nguvu na akili.

Fungua biashara hata kama ni ndogo ndogo ukiwa na kubwa ni bora zaidi.

Chagua unao waelewa waweke. My friend hutojuta. Watapata pesa , bajeti ya kula utajikuta wao ndio wanaingiza na unapata ya kusave. Utajiri utaongezeka.

Acha ubinafsi tujifunze kwa Waarabu na Wahindi.

Uza hadi Mkaaa weka mtu, uza hadi Viazi agiza mtu wa kuvifata mashambani, Uza Samaki weka mwingine wa kuzifata sokoni na feli, kama una nafasi na unapenda kufuga Weka mradi wa kuku, kuna mtu atakua kazi yake kuamka asubuhi kusafisha na kulisha kuku na jioni hivyo hivyo.

Kama una kauwezo na uba eneo na chanzo cha maju lima Mboga mboga......hutakuwi kununua mchicha wala tembele.

Braza hiyo nu fursa. Wao watapata kipato na wewe utabarikiwa.
 
Simple solution nunua au kodisha shamba asubuhi ukienda kazini toa maagizo wakalime au kupalilia, fuga kuku wa mayai au nyama waanze kuwahudumia malipo mnaelewana akizingua kata mshahara, mbona watakimbia wenyewe tu😂😂
 
Kua na pesa nyingi bank ina ladha gani ikiwa ndugu zangu ni hohehahe
Aina ladha .

Ila pia nadhani watu hasa sisi wabantu , tunabidi tuelewe utofauti wa kuwa na hela nyingi kama Currency na kuwa na Mali .

Kukaa na ndugu haimfanyi MTU akose Mali Ila inaweza ikapunguza pesa bank.

Pia hela ambayo IPO imelala bank haijalishi unaitumia au hautumii huwa inashuka thamani na sio kuongezeka thamani .

Hivyo badala ya kukaa na hela nyingi bank waweza kuwekeza katika Assets Kama mashamba , ufugaji , apartment n.k then hao hao ndugu zako ukawapa ajira kupitia project zako.


Sasa ikiwa MTU hawezi kufanya monetization kumgeuza MTU kuwa pesa maana yake hata angekaa bila ndugu asingeweza kuwa wealthiest person ever . kwakuwa kilichopo nyuma ya utajiri wa MTU sio pesa zilizopo bank Ila investment zake ambazo zinampatia returning according to the time and space.

Hata hapa hakuna MTU ambaye anakula hela za Babu yake alizoacha bank Ila tunakula Mali alizoacha babu Kama mashamba , apartment n.k.


Hivyo MTU asilialamike kuwa mshahara wake unaishia kusaidia ndugu Ila ajaribu kufikiria nawezaje kuwatumia hawa ndugu Kama fursa .
 
Kuwa Mjanja......kuwa kama Mhindi, acha kulalamika.

Mhindi unakuta Mwenye hela n mmoja lajini anaishi na Watu zaidi ya 20 nyumbani kwake. Hadi watoto wa Binamu.

Anafanikiwa vipi?

Mostly ni vijana wametoka familia duni lkn wana nguvu na akili.

Fungua biashara hata kama ni ndogo ndogo ukiwa na kubwa ni bora zaidi.

Chagua unao waelewa waweke. My friend hutojuta. Watapata pesa , bajeti ya kula utajikuta wao ndio wanaingiza na unapata ya kusave. Utajiri utaongezeka.

Acha ubinafsi tujifunze kwa Waarabu na Wahindi.

Uza hadi Mkaaa weka mtu, uza hadi Viazi agiza mtu wa kuvifata mashambani, Uza Samaki weka mwingine wa kuzifata sokoni na feli, kama una nafasi na unapenda kufuga Weka mradi wa kuku, kuna mtu atakua kazi yake kuamka asubuhi kusafisha na kulisha kuku na jioni hivyo hivyo.

Kama una kauwezo na uba eneo na chanzo cha maju lima Mboga mboga......hutakuwi kununua mchicha wala tembele.

Braza hiyo nu fursa. Wao watapata kipato na wewe utabarikiwa.
Shida sikila mtu huweza simamia BIASHARA
 
Utajiri sio wingi wa pesa, utajiri ni namna ya kujua kutatua changamoto za watu zikunufaishe.

Kadri unavyozidi kumanage matatizo ya watu wengi ndivyo unavyozidi kuwa Tajiri

Utaanza na familia yako, kisha watu wengine wasiokuhusu watakutegemea utatue matatizo yao ndio uwe tajiri zaidi

Mfano Samia anatatua matatizo ya watu milioni 60 ukiwemo wewe na hao ndigu zako yeye ndiyo kakupa hiyo ajira

Bakhresa anatatua matatizo ya watu zaidi ya milioni 90 anawafatia ngano Canada anawaletea Tz, Rwanda, uganda n.k


Anawasaidia watu wa Dar na mikoani wasioweza kwenda uwanjani waangalie mpira kwenye TV

Wewe unashindwa kutatua shida ya ndugu zako wanne utakuaje Tajiri, balozi wa nyumba kumi mbubge au waziri au Raisi?

Changamoto au matatizo ni kitu kizuri vitakuletea stress na kukukomaza akili ili uvitatue ukue zaidi uache historia na jina watu wakukumbuke kwenye ukoo wako nchi nzima, afrika au dunia yote
Kama ana biashara awarumie kama cheap labour,wamsaidie dukani au shamba
 
Ili uwatoe kwenye uhohehahe inabido kwanza ujijenge -- ukishazipata ndo unawatoa kwenye uhohehahe
Utatoaje msaada bila kujijenga? Au unamaanisha kua na maghorofa, luxury cars,
Nikipata hata 20k tu huwa siwezi kuila peke yangu yote
 
Ukiona wamekuwa wengi kwako hawana kazi anzisha Banda la kuku na Mbuzi mmoja asubuhi anakusanya mayai ya kuku mwingine anashinda anakwenda kuchunga Mbuzi.
Unaanzisha na bustani ya mbogamboga mmoja kazi yake kumwagilia bustani na kusupply mchicha na nyanya chungu kwa majirani.

Unapata labour force bila kulipia win win situation.

Watu wenye muda usio na matumizi huwa hawafukuzwi unatafuta tu matumizi ya muda wao.
Achukue ushauri huu,kama ni wavivu watajifukuza wenyewe!!
Hakuna haja ya kuwafukuza,anzisha bustani ya mbogamboga matuta ya kutosha,yamwagiliwe asubuh na jioni,pembeni kuna mabanda ya kuku yasafishwe asubuh na kuku wapewe chakula,kama ndugu ni wengi ongeza na Banda la ng'ombe WA kisasa anatakiwa kulishwa na kukamuliwa asubuh na jioni na maziwa yasambazwe kwa wateja🤓🤓🤓🤓🤓
Hapo hela inayopatikana watajilisha na kujihudumia,wavivu watajifukuza wenyewe!!
 
Kua na pesa nyingi bank ina ladha gani ikiwa ndugu zangu ni hohehahe
Ukiwa na uwezo unaweza kuwasaidia ndugu zako kuwapa,Elimu,Ujuzi,maarifa au mtaji,
Lakini sio tu kuwalea tu kama watoto wadogo,

Ukifariki wataishije ikiwa wamesha zowea kuishi kwa utegemezi?

Kila mtu ajiandae au aandaliwe ili kuja kujitegemea yeye mwenyewe,
Hao ndugu watakujaje kua na familia zao ikiwa hawana akili ya kujitegemea au kujitimizia majukumu yao wao wenyewe?

Huyo ndugu mwenye uwezo siku akianguka kifedha,ina maana familia nzima inakua imeanguka?
Tajiri anatakiwa atengeneza matajiri wengine katika familia yake ili hata kama atakuja kuanguka,kuwe na mtu wa kuja kumpa support,

Hata vitabu vya dini vinatuambia kua,Asiye fanya kazi na asile.
 
Achukue ushauri huu,kama ni wavivu watajifukuza wenyewe!!
Hakuna haja ya kuwafukuza,anzisha bustani ya mbogamboga matuta ya kutosha,yamwagiliwe asubuh na jioni,pembeni kuna mabanda ya kuku yasafishwe asubuh na kuku wapewe chakula,kama ndugu ni wengi ongeza na Banda la ng'ombe WA kisasa anatakiwa kulishwa na kukamuliwa asubuh na jioni na maziwa yasambazwe kwa wateja🤓🤓🤓🤓🤓
Hapo hela inayopatikana watajilisha na kujihudumia,wavivu watajifukuza wenyewe!!
Hhaahh
 
Back
Top Bottom