Kwa MKRISTO: Umasikini wa kipato/Fedha/Mali ni matokeo ya Shambulizi la KIROHO

Kwa MKRISTO: Umasikini wa kipato/Fedha/Mali ni matokeo ya Shambulizi la KIROHO

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
9,514
Reaction score
23,523
Kuishiwa na KUWA ombaomba sio mpango wa Mungu KWA MKRISTO.

Kwa hiyo huwezi kujisifia kuishiwa, mbango wa Mungu ni watu wasiwe tegemezi kiuchumi KWA wateja wao ( wasiomuamini Mungu).

Msisitizo uliotolewa.

1: Umasikini ni laana ( Torati 28).
Yesu ametukomboa na laana ya TORATI.

2: Mcha Mungu hatakiwi KUWA muhitaji na tegemezi kifedha. Anakumbushwa kufanya biashara ili asiwe tegemezi.
1 Wathesalonike 4
11 Tena mjitahidi kutulia, na kutenda shughuli zenu, na kufanya kazi kwa mikono yenu wenyewe, kama tulivyowaagiza;
12 ili mwenende kwa adabu mbele yao walio nje, wala msiwe na haja ya kitu cho chote.

3: Kazi ya Shetani ni Kuiba, kuharibu na kuua. Kuishiwa no USHAHIDI Kuna KITU kimeibiwa, Kuna eneo la kifedha limeuwawa.


Lengo la Uzi huu ni utambuzi. Kutambua Hali uliyo nayo sio mpango wa Mungu. Na ni kuondoka upotofu KUWA umasikini ni ukiroho. Na KUWA na Mali ni ushetani.

Pia kutambua KUMILIKI uchumi IMARA ukiwa mcha Mungu ni kutangaza vita vya kiroho na ULIMWENGU ule. Hivyo lazima ujizatiti haswa.


No hayo tu.
Mtumishi Matunduizi
 
Back
Top Bottom