Kwa mkwanja huu wa Chama na Miquissone, wewe ungeweza kubaki Simba Sc?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Wewe ungeweza? Hilo ni swali unalopaswa kujiuliza au kumuuliza shabiki wa soka au mdau anayehoji kuuzwa kwa waliokuwa nyota watatu kwenye Ligi Kuu Bara kina Luis Miquissone na Clatous Chama wa Simba na winga wa Yanga, Tuisila Kisinda.

Miquissone ameuzwa kwa mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly ya Misri wakati Chama na Kisinda wamejiunga na RS Berkane ya Morocco.

Ni kweli nyota hao kila mmoja alikuwa na mchango mkubwa kwenye timu yake hususan msimu uliopita na tukianza na Chama ambaye licha ya kufunga mabao matano na kutoa pasi za mabao ‘asisti’ tatu kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika na kuifanya Simba ifike robo fainali ya michuano hiyo kwa msimu uliopita, pia aliibuka kinara wa asisti kwenye Ligi Kuu Bara akitoa pasi za mabao 15 na kupachika mabao manane.

Miquissone naye alikuwa moto akifunga mabao matatu na kuasisti mara tatu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, huku akifunga mabao tisa na ku-asisti mara 10 Ligi Kuu Bara.

Kwa upande wa Kisinda alikuwa na msimu mzuri ndani ya Yanga akifunga mabao

matano na kutoa asisti tano kwenye Ligi Kuu Bara na kuisaidia timu yake kumaliza ligi katika nafasi ya pili.

Kila shabiki alitamani kuwaona nyota hao wakisalia katika vikosi vyao msimu ujao, lakini wameuzwa. Sio kuuzwa tu, bali wameuzwa kwa pesa ndefu ambazo Kibongo ni ngumu kwa kiongozi yeyote wa soka kuziacha

Nje ya kuuzwa kwao, ikumbukwe soka ni biashara na ndio kitu pekee wanachotegemea wachezaji kwa kiasi kikubwa kuendesha maisha na familia.

Kupitia makala hii, Mwanaspoti linakuletea uchambuzi wa mauzo ya wachezaji hao na faida zitakazopata pande zote tatu - kwa maana ya wachezaji, klabu walizotoka na wanakoenda kisha kupitia namba zilizopo hapa chini utatujibu kuwa wewe ungekuwa Yanga au Simba ungeweza kuwabakisha?

LUIS MIQUISONE
Taarifa lilizonazo Mwanaspoti ni kwamba, Miquissone ameuzwa kwa Al Ahly kwa Dola 1,000,000 ambazo ni zaidi ya Sh2.3 bilioni na atakuwa akipokea mshahara wa Dola 34,000 kwa mwezi sawa na Sh80 milioni - pesa ambazo kwa msimu uliopita zingeweza kulipa mishahara ya kikosi chote cha Simba.

Nje ya mkwanja huo, pia imeelezwa Miquissone atakuwa anapewa Dola 20,000 (sawa na Sh46.3 milioni) kama bonasi ya kufanya manunuzi yeye na familia yake. Hapo bado hayajatajwa marupurupu mengine atakayoyapata akiwa ndani ya Al Ahly. Hilo ndilo dili la thamani kubwa kufanywa na Simba tangu kuanzishwa kwake, je Simba wangekataa ofa hiyo?

CLATOUS CHAMA
Kabla ya kuonekana akiwa amevalia jezi ya RS Berkane sambamba na Kisinda, kiungo huyu fundi alikuwa kwenye mawindo ya Far Rabat ya nchini Morocco inayonolewa na kocha wa zamani wa Simba, Sven Vandenbroeck.

Inaelezwa kuwa Far Rabat ilikuwa tayari kutoa Dola 600,000 (sawa na takriban Sh1.3 bilioni) kama ada ya uhamisho, lakini dili hilo likapigwa chini na mabosi wa Simba na kuamua kumpiga bei RS Berkane.

Kwa mantiki hiyo huenda Simba imelipwa pesa zaidi ya Sh1.3 bilioni kumuachia Chama na taarifa za ndani ni kwamba, kambi ya Simba inayoendelea Morocco ni moja ya makubaliano yaliyofanywa na pande hizo mbili katika dili la Chama.

My Take
Nakuuliza wewe shabiki maandazi ungeweza kubaki Simba Sc?
 
Hiyo dili ni nzuri hata kina Neymar, Messi, Ronaldo waliondoka kwenye timu zao wakiwa kwenye peak. Chama na Miquison wapo vizuri na pia walioingia Simba ni wazuri pia, hizo nafasi zao zinaweza kuzibwa au hata zaidi yao.
 
Hiyo dili ni nzuri ,hata kina Neymar,Messi ,Ronaldo waliondoka kwenye timu zao wakiwa kwenye peak .Chama na Miquison wapo vizuri na pia walioingia Simba ni wazuri pia ,hizo nafasi zao zinaweza kuzibwa au hata zaidi yao.
Amekwambia nani mapengo yao yanaweza kuzibwa.?

Mpaka leo pengo la Okwi (Winga wa kushoto) bado halijaweza kuzibwa vyema. Morrison ndio tia maji tia maji katika eneo lile. Lakini bado hajaweza kuimudu nafasi vyema.
 
Kwa hiyo baada ya mauzo, hela za hao wachezaji zimeingizwa kwenye akaunti ipi? Ya Moo au ya klabu? Na mchanganuo wake ukoje?

Nimeuliza hivi, kwa sababu kwa upande wa Kisinda wa Yanga, Katibu wao alishatolea maelezo juu ya mchanganuo wa fedha za mauzo yake. Hivyo nahitaji majibu yenye weledi! Na siyo yale ya kila siku ya kimbumbumbu.
 
Huwezi kupata majibu ya kiweledi sababu swali lako ni la kimbumbumbu. Unataka simba watoe mchanganuo kisa yanga washatoa, sasa huo ndio umbumbumbu wenyewe.
 
Pesa zitakuwa zimeingia account ya Mo ukwaju.
 
Kuna dili limefanywa wanamsimbazi watalia. Ile sarakasi ya Ramadhan Wasso inakuja kujirudia. Kuna mchezaji atatambulishwa mwishoni kwa wananchi siku watu watazimia. Wacha niishie hapo.
 
Unajifanya unaakili kumbe mbumbu tu hujui lolote kuhusu mfumo wa uwekezaji ndani ya Simba upoje. Watanzania tumejaa wivu kaa mbwa vile. Account ya club unaijua, signatories unawajua? Kampuni inayomiliki Simba unaijua. Jiulize Chelsea ikafanya mauzo ya wachezaji, matangazo na asset zingine hela zinaonda wapi mfokoni wa boss au lah. Fanya utafuti kuelewa Mambo uselete njaa zako muhamedi yuko pale kutengeneza faida na ndio dunia ya leo ya capitalism, ndio maana kaweka mtaji ili kuleta progress na sio uswahili kujifanya mnajua kumbe wajinga tu
 
Povu la nini sasa!! Nilitegemea ujibu kama mtu mwenye weledi. Ila kwa bahati mbaya umejibu kama barbara vile!
 
mmoja kati ya hao wawili kesha sajiliwa Yanga, na ndiye atakuwa wa mwisho kutambulishwaaaaaa!
 
Mbona hamuulizi hela za kuwanunua zilitoka kwenye akaunt ya nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…