Kwa mliooa tukutane hapa

Kwa mliooa tukutane hapa

thirteen06

Senior Member
Joined
May 17, 2021
Posts
118
Reaction score
100
Kwenye kusaka mwenza utata ni mwingi Sana. Unaweza fika mahali ukahisi kuchoka kuhangaika kutafuta mwenza wa ndoto zako ili kupata alie Bora, matokea yake wote unaowachunguza kwa lengo zuri la kuoa unakutana na sintofaham mbalimbali ambazo ukizifikiria kwa undani unaona kabisa baadae unaweza kupata changamoto nyingi endapo utaridhia kukamilisha taratibu za uchumba na kuoa.

Wakati mwingine utakutana na watu watakwambia usichunguze sana hakuna aliyekamilika na tena anaweza kuongezea kabisa kwamba ukimchunguza Sana Bata huwezi kumla na kwamba hakuna aliyekamilika.

Je mlioingia kwenye mahusiano ya mume na mke "anyway" yaani unamashaka lakini unahisi Kama umechoka kuchunguza mana kila unayeanzisha nae mahusiano Ni hola, then ukaamua tu kuoa ivo ivo mnasemaje kuhusu hili?
 
Preference zako kwa mahusiano ni tofauti na za wengine, vigezo vyako vya mke bora haviwezi kuwa sawa na vya mwingine kwa hiyo cha kukushauri wewe anglia unaeona anakufaa na amekidhi vigezo vyako weka ndani

Ukisema kila mtu aseme experience yake hapa, mwingine atakwambia alipenda tu kucha akaamua kuoa, mwingine atasema amempendea tabia, mwingine atasema amependa macho yake, mwingine atakwambia mke wake ana akili kwa hiyo ameoa ili apate watoto wenye akili na kuna wanaume wa Dar watakwambia wife kwao wana uwezo kwa hiyo ameoa ili apate urahisi wa maisha

Sijui umeelewa lakini, au niongeze sauti Anyways, wenye wake zao wanakuja
 
Preference zako kwa mahusiano ni tofauti na za wengine, vigezo vyako vya mke bora haviwezi kuwa sawa na vya mwingine kwa hiyo cha kukushauri wewe anglia unaeona anakufaa na amekidhi vigezo vyako weka ndani

Ukisema kila mtu aseme experience yake hapa, mwingine atakwambia alipenda tu kucha akaamua kuoa, mwingine atasema amempendea tabia, mwingine atasema amependa macho yake, mwingine atakwambia mke wake ana akili kwa hiyo ameoa ili apate watoto wenye akili na kuna wanaume wa dar watakwambia wife kwao wana uwezo kwa hiyo ameoa ili apate urahisi wa maisha


Sijui umeelewa lakini, au niongeze sauti
Anyways, wenye wake zao wanakuja
upo sahihi kabisa
 
Majuzi ijumaa nilienda kumuona babu akaniambia mbona unachelewa kuoa nikamwambia bado namchunguza akacheka sana akaniambia huwezi kumchunguza mwanamke maana hutaona baya kwa sasa ila ukishaoa ndo utajua ukweli wake halisi kama sio mke kutoka kwa Mungu utaimba hallelujah tu kikubwa omba mke mwema basi kumchunguza mtu ngumu.
 
Back
Top Bottom