johnmashilatu
JF-Expert Member
- Sep 16, 2010
- 1,263
- 1,753
Jana nimepanda coaster inayotoka Airport kuelekea Buhongwa jijiji Mwanza, ambapo niliona ubunifu wa CDM kuwafikia watu wengi hasa katika hii Kampeni ya NRE.
Nilivyoingia nilikuta ukimya, huku sauti ya John Heche ikisikika vyema. Awali nilifikiri ni msafiri anacheza clip kutoka kwenye simu yake.
Haikuwa hivyo, abiria katika Coaster hii iliyokuwa imejaa, walikuwa wakisikiliza hotuba ya Heche aliyoitoa Mkoani Mbeya wakati wa ziara yao ya NRE.
Mara kadhaa nilishuhudia abiria wakipiga makofi, kufurahia au kujibu hotuba hiyo hasa pale Heche alipokuwa akiuliza huu sio ufisadi..
Kwangu mkazi wa maeneo ya vijijini hili likuwa geni kwangu, nikajiuliza kuwa teknolojia inafanya mambo makubwa, hakuna ulazima tena kutaka nyomi kiwanjani, kama una madini watakusikiliza popote na ujumbe utafika.
Kwa takriban saa moja na ubovu wa barabara hasa maeneo ya mkuyuni, umma huu ulikuwa uiiguatilia hotuba hii kwa makini kabisa.
Nikajiuliza itakuwaje robo ya bodaboda nchini wakawa na hotuba hizi, vipi robo ya daladala zikawa na hotuba hizi? ujumbe utawafikia watu wangapi? Aliyebuni huu mkakati wa kurekodi hotuba hizi na kuzisambaza aliona mbali.
Muliro anaweza kuzuia mkutano wa hadhara usifanyike, watu wakajifungia chumbani, wakarekodi na ujumbe ukasambazwa!