Hatari Sana, ndio maisha wengi wanaishi. Vyumba kumi na ushee, tena Choo kimoja Tu. Ukiwa bachelor unayeanza kujitafuta na akili isiyo na mambo mengi unaweza usione tabu sana, mziki upo pale Una familia tena ya watoto na chumba ni kimoja tu huwa inaumiza Kwa mpambanaji na inaweza kukuongezea mzuka wa kutafuta zaidi...
Changamoto zake nahisi zitakuwa pia kwenye bills na usafi wa nyumba (ndani), Choo na hapo kwenye korido, kitu kingine ni privacy hapo hakuna kujiachia, hata ukiwa ndani ww na mkeo unasubiri watu wote walale au unafungulia mziki mkubwa ili mmalize Jambo lenu, malezi pia yatakuwa kwenye changamoto.
Umaskini unatisha Sana, lazima uwe na maarifa pamoja na juhudi zenye akili ili utoke kwenye mazingira ya Aina hiyo.