Kwa moto anaouwasha Khaligraph Jones Wanahip hop wakubali kuwa wana mengi yakujifunza toka kwake

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
4,869
Reaction score
13,137
We talk about Consistency(muendelezo). mkubwa Papaa Jones anawasha moto since day one kiukweli tukiweka uzalendo pembeni kwa bongo hii nani tunaweza kumuamini akabattle na Khaligraph?

Mimi ni mshabiki mkubwa wa Fid q anafanya vizuri kwa upande wake but tukiongelea International Papaa Jones yupo ahead kuliko GOAT wetu wa Hip-hop Tanzania. Sasa nani hapo tumlinganishe na Papaa Jones je ni Young Killer, Young Lunya, Songa, Rapcha, Dizasta au nani?

Mtu anapo kuambia ukweli doesn't mean amekudharau.
 
Sio kwa sababu ana rap kiingereza bali ni kwa sababu anafanya vizuri international na muendelezo wa kutoa jiwe juu ya jiwe investment ya uhakika kwenye audio na video.
Mtu hata akienda kufanya show Malawi hiyo nayo pia ni international

Hata kina Songa wanakubalika sana Kenya na wana Collabo nyingi na wasanii wa huko

Na hata huyo Khaligraph ameanza kusikika baada ya yeye kujifunza kwa Tamaduni.
 
Huyo Mex Cortez ni kiumbe mwingine

Naamini mwamba ni mmoja wa kumchallenge Kaligraph ni Nikki Mbishi nasubiri tu Baba Malcom aingie booth atoke na mawe ila Roza Ree nimemkubali
Wakum Challenge sio mmoja labda tu watu waamue kuficha silaha zao watulie.

"Yes Bana" yake tu aliyoifanya bado haijawa kali kuliko Challenge ya yes Bana aliyofanya Mawenge.

Mawenge kupitia Yes Bana challenge kakusimulia stori ya kurasa tatu kwa dakika moja

Nambie kwenye yes Bana ya Khaligraph kuna lyrical gani mle?
 
Jones yupo vizuri!! namwelewa ila kwa hiki alichokitafuta TZ. amelikoroga 📢📢ni muda wakufungia vijibwa ndani ...
Natangaza rasimi mlango wa majibwa umefunguka...💀🦴🦴..

Khaligraph👉🥴
 
Mtu hata akienda kufanya show Malawi hiyo nayo pia ni international

Hata kina Songa wanakubalika sana Kenya na wana Collabo nyingi na wasanii wa huko

Na hata huyo Khaligraph ameanza kusikika baada ya yeye kujifunza kwa Tamaduni.
Mkuu Kwa rappers Africa Mashariki kwa wakati huu tuliopo Khaligraph Jones katengeneza ufalme wake wasanii wetu wana kazi kubwa kufikia levels zake kuanzia hits alizonazo, numbers kwenye digital platform na mafanikio kutokana na kile anachofanya.

Songa anafanya vizuri lakini ukimlinganisha na Khaligraph Jones in general ni kutomtendea haki maana mwenzake ni Award winner
 
We talk about Consistency(muendelezo). mkubwa Papaa Jones anawasha moto since day one kiukweli tukiweka uzalendo pembeni kwa bongo hii nani tunaweza kumuamini akabattle na Khaligraph?

Mimi ni mshabiki mkubwa wa Fid q anafanya vizuri kwa upande wake but tukiongelea International Papaa Jones yupo ahead kuliko GOAT wetu wa Hip-hop Tanzania. Sasa nani hapo tumlinganishe na Papaa Jones je ni Young Killer, Young Lunya, Songa, Rapcha, Dizasta au nani?

Mtu anapo kuambia ukweli doesn't mean amekudharau.
Jones ni level za kina Billnass, Yani ni Lunya aliechangamka na Expossure. Usimlinganishe na Vichwa vya Hip hop ya 255.
 
Mkuu Kwa rappers Africa Mashariki kwa wakati huu tuliopo Khaligraph Jones katengeneza ufalme wake wasanii wetu wana kazi kubwa kufikia levels zake kuanzia hits alizonazo, numbers kwenye digital platform na mafanikio kutokana na kile anachofanya.

Songa anafanya vizuri lakini ukimlinganisha na Khaligraph Jones in general ni kutomtendea haki maana mwenzake ni Award winner
Ufalme gani?

Kuna utofauti wa kuwa maarufu na kufanya vizuri

Kuwa maarufu sio lazima ufanye vizuri kuna msanii kaimba "haniiiii" na ngoma ime hit watu wanaisikiliza.

Lakini tunapoiweka hiyo nyimbo kwenye mizani ya ubora basi uzito wake utakuwa sawa na nyoya.

Of course Khaligraph sio kama ana ngoma mbaya na wala sio kama ana ngoma nzuri kuzidi marapa wa nyumbani.

Nadhani ni ile flavour ya lugha ya kiingereza ndio inayokuja kumuongezea credit.

Hata saizi nikikuuliza ngoma gani aliyofanya Khali kwa lugha ya kiswahili ika hit utanijibu nini?

Lugha ya kiingereza ndio inayompaisha asikilizwe na kualikwa kwenye shows nje ya mipaka ya Kenya. Lakini when it comes to content and lyrical. Khali hawezi kusimama na msanii yeyote wa Tamaduni.
 
Wakum Challenge sio mmoja labda tu watu waamue kuficha silaha zao watulie.

"Yes Bana" yake tu aliyoifanya bado haijawa kali kuliko Challenge ya yes Bana aliyofanya Mawenge.

Mawenge kupitia Yes Bana challenge kakusimulia stori ya kurasa tatu kwa dakika moja

Nambie kwenye yes Bana ya Khaligraph kuna lyrical gani mle?
Ngoja tuone hii challenge itakuwa tamu sana
 
Rapa ka’ me hakuna..
Na ukibisha jitokeze… aargh!! nakutafuna
Na nikiamua nakinukisha mpaka watu wananuna.
Ila wewe kukinukisha labda uamue kun.yA 💩

😂😂 hayatuhusu, lakini challenge zinafurahisha.
 
😀😂
Screenshot_20230826_093754_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom