Kwa moto anaouwasha Khaligraph Jones Wanahip hop wakubali kuwa wana mengi yakujifunza toka kwake

Vichwa kama vipi?? Numbers hazidanganyi mkuu anachofanya Jones ni kitu kizuri ndio maana anafanya vizuri
Kweli anafanya Vizuri in terms of Popularity lakini kwa issue ya Content na Flow uyo ni level za kina Chin beez siwez mconpare hata na Songa achilia mbali Dizasta na Fid Q
 
Atleast ungezungumzia content na sio flow ukija kwenye flow ni mtu anayebadilika na mwenye maujanja(swagger).

Unapokubalika na wengi tafsiri ya kawaida ni kuwa unafanya vizuri sasa kwa nini wakina Songa na Dizasta licha ya kuwa bora kwa kile wanachokifanya still numbers zao haziridhishi hawatengenezi Fanbase mpya?
 
Tutegemee kitu tena,

Nilichogundua kwenye pin la khaligraph kaianda kitambo ndo katoa shombo .

Kali Anarudi tena chimbo tutegemee kitu hapa
 
Attachments

  • Screenshot_20230826-115322_X.jpg
    Screenshot_20230826-115322_X.jpg
    529.3 KB · Views: 4
Ufalme gani?

Kuna utofauti wa kuwa maarufu na kufanya vizuri

Kuwa maarufu sio lazima ufanye vizuri kuna msanii kaimba "haniiiii" na ngoma ime hit watu wanaisikiliza.

Lakini tunapoiweka hiyo nyimbo kwenye mizani ya ubora basi uzito wake utakuwa sawa na nyoya.

Of course Khaligraph sio kama ana ngoma mbaya na wala sio kama ana ngoma nzuri kuzidi marapa wa nyumbani.

Nadhani ni ile flavour ya lugha ya kiingereza ndio inayokuja kumuongezea credit.

Hata saizi nikikuuliza ngoma gani aliyofanya Khali kwa lugha ya kiswahili ika hit utanijibu nini?

Lugha ya kiingereza ndio inayompaisha asikilizwe na kualikwa kwenye shows nje ya mipaka ya Kenya. Lakini when it comes to content and lyrical. Khali hawezi kusimama na msanii yeyote wa Tamaduni.
Kwani bongo hakuna marap wanaoweza kuchana kwa kiingereza kiwabebe wawe na popularity kama ya Khaligraph.?

Na sio wote wanaomsikiliza Khaligraph wanajua na kuelewa lugha ya kiingereza maana anachana kwa kiswahili pia kinachovutia kwake ni mpangilio wa flow na sound.

Wengi mnajificha kwenye kivuli cha contents kana kwamba rappers wa bongo wanafanya gospel wakati content za muziki wa rap obviously zinajulikana ni kujisifia
 
Atleast ungezungumzia content na sio flow ukija kwenye flow ni mtu anayebadilika na mwenye maujanja(swagger).

Unapokubalika na wengi tafsiri ya kawaida ni kuwa unafanya vizuri sasa kwa nini wakina Songa na Dizasta licha ya kuwa bora kwa kile wanachokifanya still numbers zao haziridhishi hawatengenezi Fanbase mpya?
Nadhani shida ya Rappers wazuri wa TZ ni uwekezaji tu na kutokua committed basi. Bado wana ile wakiwezeshwa wanaweza they cant stand alone.
 
Bongo hiphop tuna Wasanii wengi wakali, labda kuliko hata Khaligraph, ila wako wapi now? hawaendi popote. Yanabaki majina yao tu.

Ni kama bongoflava pia, wasanii wengi tunawasifu sana ila nje ya hapa Bongo hawaendi popote.

Nchi nzima msanii nayevuka boda ni Diamond peke yake, kidogo na vijana wake. Bado tuko nyuma sana.
 
Kwani bongo hakuna marap wanaoweza kuchana kwa kiingereza kiwabebe wawe na popularity kama ya Khaligraph.?

Na sio wote wanaomsikiliza Khaligraph wanajua na kuelewa lugha ya kiingereza maana anachana kwa kiswahili pia kinachovutia kwake ni mpangilio wa flow na sound.

Wengi mnajificha kwenye kivuli cha contents kana kwamba rappers wa bongo wanafanya gospel wakati content za muziki wa rap obviously zinajulikana ni kujisifia
Kuhusu lugha

Unachoshindwa kuelewa ni kuwa mashabiki wako wa kwanza lazima wawe wale wakaribu.

Hata wewe leo uanze muziki lazima watu wako kutoka mtaani ndio utaokuwa wakwanza kuwaangalia kama mashabiki.

Sasa Tanzania hapa lugha ya kiingereza bado haijapewa kipaumbele tofauti na wenzetu Kenya ambapo hata mtu ambaye hajui kusoma mnaweza kuzungumza kiingereza vizuri mkaelewana.

Marapa wa Tanzania wangechana Kiingereza basi hata sisi tusingewajua kwasababu wasingepewa time na mashabiki.

Ila wangekuwa favoured na Taifa iwapo tungekuwa ni Taifa linalozungumza Kiingereza.
 
Kwani bongo hakuna marap wanaoweza kuchana kwa kiingereza kiwabebe wawe na popularity kama ya Khaligraph.?

Na sio wote wanaomsikiliza Khaligraph wanajua na kuelewa lugha ya kiingereza maana anachana kwa kiswahili pia kinachovutia kwake ni mpangilio wa flow na sound.

Wengi mnajificha kwenye kivuli cha contents kana kwamba rappers wa bongo wanafanya gospel wakati content za muziki wa rap obviously zinajulikana ni kujisifia
Flow ndio nini?

Flow hutegemeana na category ya Hip Hop unayo rap.

Khali ni Afro Rapper aina yake ya uchanaji kupitia category hiyo ndio inayomlazimisha awe na flow nzuri.

Ushamsikia Joyner Lucas?

Kwako wewe huyu utaona sio msanii mkali kwasababu hana flow kumzidi Offset?

Kujisifia ni part of content na ni role ya rapper while kuelimisha ni role ya mcee.

Kujisifia anakojisifia Young Lunya huwezi fananisha na kujisifia anakojisifia Dizasta kwenye series ya Nobody is safe.

Hapo nimezungumzia weak verses.
 
Una maoni gani hapo. 🤣🤣 yani motraa tayari ameanza kumjambisha mshikaji ila huyu khali ajitathimini kwanza🤭
 
Kwani bongo hakuna marap wanaoweza kuchana kwa kiingereza kiwabebe wawe na popularity kama ya Khaligraph.?

Na sio wote wanaomsikiliza Khaligraph wanajua na kuelewa lugha ya kiingereza maana anachana kwa kiswahili pia kinachovutia kwake ni mpangilio wa flow na sound.

Wengi mnajificha kwenye kivuli cha contents kana kwamba rappers wa bongo wanafanya gospel wakati content za muziki wa rap obviously zinajulikana ni kujisifia
Shida wa Tanzania wengi wanaleta ushabiki kwenye vitu vya msingi kiuhalisia jones anatubeba east Africa when it comes to hip hop, jones ndo anaweza kwenda sambamba na akina Mnyama sarkodie, tukiweka ushabiki pembeni wasanii wa hip hop bongo wana la kujifunza kwa papas jones
 
Bongo hiphop tuna Wasanii wengi wakali, labda kuliko hata Khaligraph, ila wako wapi now? hawaendi popote. Yanabaki majina yao tu.

Ni kama bongoflava pia, wasanii wengi tunawasifu sana ila nje ya hapa Bongo hawaendi popote.

Nchi nzima msanii nayevuka boda ni Diamond peke yake, kidogo na vijana wake. Bado tuko nyuma sana.
Ukisoma comment unagundua tatizo lilipo, ujuaji mwingi sisi wa Tz hatupendi kukubali pale tunapozidiwa lazima tutoe execuses, na hatutaki kujifunza, kihulasia kwa sasahivi jones amesogea
 
Back
Top Bottom