Kwa mpira huu wanaocheza Ubelgiji nawashauri wasiende Qatar kuepuka aibu

Kwa mpira huu wanaocheza Ubelgiji nawashauri wasiende Qatar kuepuka aibu

Execute

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2022
Posts
3,000
Reaction score
7,336
Naangalia mechi kati ya Misri na Ubelgiji hapa na ninaona hawa Wabelgiji warudi nyumbani kwao kuepuka dhahama kwenye Kombe la Dunia.

Beki zinakatika na kutoa maboko, haziwezi kufanya marking wala kukaa man to man.

Forward hazifanyi attempt yoyote zaidi ya kupiga back pass.

Wameshapigwa 2 bila.
 
Mkuu mtoa mada soma hii na tunza, Belgium 🇧🇪 world cup hii imeshindwa sana itaushia semi final
Mpira unadunda hivyo lolote laweza kutokea. Walipomtoa hazard angalau mpira ulibadilika kidogo.

Ila hawana aggressiveness kule mbele na beki zao zimetoboka. Bado siwaoni wakivuka 16 bora.
 
Usisahau hiyo mechi ni kwa ajili tu ya kutest mitambo. Wachezaji wengi watakuwa wanacheza kwa tahadhari kubwa, ili wasije wakapata majeraha dakika za lala salama, na hivyo kukosa kushiriki mashindano ambayo ni ndoto kwa wachezaji wengi.
 
Mpira unadunda hivyo lolote laweza kutokea. Walipomtoa hazard angalau mpira ulibadilika kidogo.

Ila hawana aggressiveness kule mbele na beki zao zimetoboka. Bado siwaoni wakivuka 16 bora.
We can bet on this,Belgium 🇧🇪 wataenda hadi semi final, all African team zitaondolewa hatua ya mwanzo, watch out France, England 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿, Brazil kuchukua world cup 2022
 
Hivi England huwa mnaionaga ni timu ya kutiiisha??
England ni timu yenye wachezaji wazuri sana na ilitakiwa iwe tishio. Tatizo ni kocha wao. Huyu jamaa tangu aingie kwenye nafsi ya ukocha wa timu ya England sijui hasa timu inacheza formation gani. Hata kombe la dunia lililopita walibahatisha tu. Kocha mbovu.
 
Usisahau hiyo mechi ni kwa ajili tu ya kutest mitambo. Wachezaji wengi watakuwa wanacheza kwa tahadhari kubwa, ili wasije wakapata majeraha dakika za lala salama, na hivyo kukosa kushiriki mashindano ambayo ni ndoto kwa wachezaji wengi.
Aina ya makosa wanayofanya hayaoneshi kama sababu ni kuogopa kuumia. Ila ni sahihi, ngoja tusubirie world cup ikianza.
 
Yani hii timu wala huwa siiwazii, sijui ni nini ambacho huwa kinawafanya watu kuipa imani kiasi hiko? Sijawahi kuona maajabu yao zaidi ya hypes nyiiiiingiii.
Waingereza huwa wana kelele sana kwenye media ndio maana baadhi ya watu wanadhani nayo ni timu nzuri.

Ila kwa mara nyingine tena mwaka huu wanaenda world cup na wachezaji wengi wazuri.
 
Naangalia mechi kati ya misri na ubelgiji hapa na ninaona hawa wabelgiji warudi nyumbani kwao kuepuka dhahama kwenye kombe la dunia.

Beki zinakatika na kutoa maboko, haziwezi kufanya marking wala kukaa man to man.

Forward hazifanyi attempt yoyote zaidi ya kupiga back pass.

Wameshapigwa 2 bila.
Yan unawahukumu kwenye mechi ya kirafiki
Unataka watumie nguvu kupata ushindi wakat wana mechi muhimu j5
 
Yan unawahukumu kwenye mechi ya kirafiki
Unataka watumie nguvu kupata ushindi wakat wana mechi muhimu j5
Hata misri hawakuwa wanacheza mpira wa nguvu. Hapa naongelea tu ule ufundi unaoonekana pamoja na makosa yanayofanyika. Forward haina aggressiveness na beki zinakatika na kutoa maboko.
 
Mimi nawapa Argentina nafasi ya kwanza kubeba kombe halafu pia kuna Brazil na Portugal. Hawa wengine kama ufaransa wataishia makundi au 16 bora.

England na Spain wanaweza kufika robo au nusu fainali. Hata Senegal nategemea wafike robo hata mpaka nusu fainali.
Hakuna timu ya africa inafika robo😂
huu ni ukwel mchungu,
 
Back
Top Bottom