Kwa mpira wa jana mapengo ya Chama na Miqueson yapo wazi

Ratcha

Senior Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
129
Reaction score
339
Jana simba imecheza mechi ya kirafiki na kutoa sare, kwa mpira ule kocha anakazi ya ziada kukijenga kikosi, tumefungwa magoli ya offside alafu mpira tumecheza kama chandimu, nimeamini itatuchukua muda kuyaziba mapengo ya chama na luis

Nb: kama hujaona clip za mchezo ule katizame kwanza ndo uchangie.
 
Ivi wabongo lini tutabadirika? Huyo Chama na Konde walikuwepo tokea Simba inaanzishwa na kubeba vikombe mbali mbali ,je hao wachezaj hawazeek unataka kusema wangecheza milele Simba ili iweze kuwa Bora zaidi?

Je unajua club ya Simba inaendeshwaje?
Je ni Nan aliwaleta hao wachezaji?
Je kabla hawajafika Simba ulikuwa unajua ubora wao kabla?
Je hao wachezaj wapya umeishawapima kwa kifaa gan kuprove kuwa hawana uwezo kuzid chama na konde?

Je huo mpira wa Jana uliangalizia kwenye channel ipi ambayo wengine hatukuiona?
Je clips ndio ikufanye utoe conclusion kuwa walicheza vibaya?
Je ni timu gan mbovu inaweza kufanya comeback huku ikiwa nyuma magoli 2 kipindi Cha kwanza na kusawazisha yote kipindi Cha pili?

Unapata wap ujasiri wa kukosoa timu mapema hivyo wakat ndio kwanza wachezaj walio wengi ni wapya hivyo wanahitaj kujuana zaidi na kwenda na mfumo wa mwalimu kwa pamoja?

Je nikisema wewe ni utopolo ntakuwa nakosea ?

Vipi unaweza kunitajia timu yoyote dunian ambayo haijawah kufungwa Wala kutoa draw?
Why Simba kila Mara?

Je wakukabidhi club ya Simba ikiwa na konde na chama alafu utuhakikishie kuwa timu itakuwa Bora milele yote na kubeba vikombe kinyume na hapo u sign mkataba kuwa timu isipofanya vizur nipigwe shaba ya matako.
 
Mechi moja isikupe picha kwamba timu iko katika hali gani, timu bado iko katika mfumo wa kusomana na kuelewana baina ya wachezaji wapya na wageni

Mbele ya safari huko mambo yatakuwa bam bam

Usiogope!
 
Mmefungwa au mmefunga magoli ya offside?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23]
 
Kwahiyo pengo la chama lilikuwa wapi pale?
Mtu umeangalia highlight unaanza kusema kuna pengo.....
Yes, mfano kuwe na pengo unapendekeza nini kifanyike?
Timu haikua na utulivu, inshort walikua wanafika ruka tu, kwa sasa simba tunahitaji utulivu sana ili team yetu ipate muunganiko
 
Ivi wabongo lini tutabadirika? Huyo chama na konde walikuwepo tokea Simba inaanzishwa na kubeba vikombe mbali mbali ,je hao wachezaj hawazeek unataka kusema wangecheza milele Simba ili iweze kuwa Bora zaidi?..
povu ruksa
 
"Hii ni takatakaa" in Raila odinga voice
 
Umeona full mechi au highlights tu Mkuu?
 
Clip ya dakika mbili kwako ilitosha kabisa kuona pengo la chama na Luis.

Timu imefanya usajili wachezaji ndiyo mechi yao ya kwanza wewe umeona pengo la chama ?

Tena unakuja kuanzisha uzi kama hamna kazi zingine za kufanya muwe mnaona aibu kupost ujinga.
 
Ukiangalia kwa umakini utagundua wale wamorocco waliweka highlights zao tuu simba wakaweka magoli tuu maana wao ndio walikua wanamaamuzi nini waweke na nini wasiweke kwenye highlights.
 
Wewe utakapo badilika wabongo tutabadilika
 
Muda ni mwalimu mzuri utatujiby kwa usahihi zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…