Hakuna ubishi jana tumeionyesha Afrika na Dunia kuwa sisi soka bado saana. Mambo machache niliyoyaona mimi kweny emchezo wa jana na ambayo yamekuwa yakijirudia rudia:
1. Wachezaji hawana kabisa misingi muhimu ya uchezaji mpira mfano jinsi ya kumiliki mpira, kufanya maamuzi yenye tija na malengo pamoja na kuwa na kuwa wengine wanacheza nje ya nchi .
2. Nina wasi wasi na walimu wa soka letu kuanzia vilabu mpaka timu ya Taifa sijui wanawafundishaga nini hawa wachezaji wetu...sawa kuna vitu vingine ni '"basic" mchezaji anatakiwa kuvijua mapema lakini swala la malengo ya mchezo hiyo ni kazi ya mwalimu.
3. Lishe bado ni tatizo kubwa saana kwa wachezaji hasa wa ukanda huu wa Africa Mashariki .Wapo wanaolalamikia maumbile ya wachezaji wetu kwamba madogo lakini hili sio tatizo kuna tofauti kati ya maumbile na lishe .Angalia wachezaji wa Korea na Japan au Mexico wengi wao tunafanana maumbile au tunawazidi kimo lakini bado wana stamina. Sisi chips kavu zinawamaliza wanamichezo wetu!
4. Haya matitizo bahati mbaya hayawezi kurekebishika au kutatuliwa kwa wachezaji tulionao sasa, tayari mda umewakimbia. Kazi kwetu kama tunataka kusonga mbele tuanze upya kwa kuwekeza kwenye vijana lakini pia na kutafuta walimu wanaolijua soka na waliotutangulia kwenye mpira na sio kupeana nafasi za ukocha kisiasa. Nimeambiwa "under 20" eti mwalimu ni Julio! Maweeeeee!!
5.Mwisho kabisa tunatakiwa kuwa na viongozi wa soka sio wenye nidhamu tu kama ilivyo sasa bali wawe wanalijua soka na misingi yake vinginevyo ni aibu tu.
Ngoja nisubiri kuwasikiliza wachambuzi wetu wa soka kuona jinsi watakavyofunguka kuhusu "performance" ya timu yetu kama wanavyofungukaga kwenye mechi za Simba na Mtibwa au Yanga na Gwambina.