Kwa mshahara wa laki saba naweza kujenga nyumba?

MUBIKU

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2014
Posts
283
Reaction score
384
Habari za majukumu wakuu,

Naomba mwenye ujuzi na uzoefu juu ya masuala ya ujenzi anisaidie. Nahtaji kujenga nyumba ya vyumba vitatu kiwanja tayari ninacho na mshahara wangu ni laki 7 kwa mwezi.

Asante na karibuni
 
Habar za majukumu wakuu , naomba mwenye ujuz na uzoefu juu ya maswala ya ujenzi , nahtaji kujenga nyumba ya vyumba vitatu kiwanja tayari ninacho, na mshahara wangu ni laki 7 kwa mwez. asante na karibun
Kwahiyo huo mshahara wako huutumii kwa kula mavazi usafiri,refreshment, matibabu na sadakah. Niwakujenga tu. au?
 
Habar za majukumu wakuu , naomba mwenye ujuz na uzoefu juu ya maswala ya ujenzi , nahtaji kujenga nyumba ya vyumba vitatu kiwanja tayari ninacho, na mshahara wangu ni laki 7 kwa mwez. asante na karibun

Tiririka bajeti yako ya mwezi mzima tuone unabakiwa na kiasi gani.
Kodi ya Nyumba
Umeme
Maji
Chakula
Nauli
Matibabu
Ada za Watoto kama unao.
Menginyeo

Jumla yake............................
 
Huo mshahara ni take home au ni gross?
Una plan ya kujenga baada ya muda gani?
 
Kwa mwaka kipato chako ni 8.4m kwahiyo kama unajenga jijini Dar kwa standard za dar angalau miaka 3 utapata nyumba bila urembo (finishing nzuri) ukiwa mkoani kijijini ni mwaka moja kwa wastani wa nyumba huku......kwahiyo kama unataka tujadili vizuri tukupe na bei sema eneo lako liko wapi hata kama ni Dar osterbay Bunju au Tegeta
 
Ninamfahamu secretary mmoja serikalini analipwa 390,000/ sijui ni kabla au baada ya makato amejenga nyumba japo ametumia km miaka minne mitano hivi. Kamaliza, na alinambia hajajengewa na mtu.

So ni wewe tu namna ya kujipanga!
Usiamini vipato vya wanawake hususani ma secretary, wengi wana biashara ya siri na ma bosi...ukijilinganisha nao utaaga town jomba
 
Inawezekana ukianza kununua materials(saruji,tofali) kidogokidogo alafu unahifadhi..baadae unamalizia (bati na mbao)...hii for roof covering...hapo inakuwa imebaki finishing pia ambayo utaenda nayo taratibu finally unakamilisha nyumba
 
Habar za majukumu wakuu , naomba mwenye ujuz na uzoefu juu ya maswala ya ujenzi , nahtaji kujenga nyumba ya vyumba vitatu kiwanja tayari ninacho, na mshahara wangu ni laki 7 kwa mwez. asante na karibun
Mkuu hata mshahara wa laki nne unaweza kujenga, mm nina nyumba 2 na viwanja 2 havijajengwa na nina mshahara kama wako, natembelea gari pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…