Pamoja na ushauri wote wa mapato na matumizi, kibongobongo wengi wetu tumejenga kwa kuangalia hitaji la wakati husika.
Ushauri wangu ni kuwa Ujenzi wetu wa kipato cha chini huo tunaufanya kwa kugawanya hatua za ujenzi katika awamu kama ifuatavyo:
1. Anza kununua mabati.
Hii ni muhimu sana maana nyumba ikisha pauliwa inatakiwa iezekwe haraka vinginevyo mbao za paa zitapinda.
2. Uliza gharama za kusafisha uwanja. Ukipata changa pesa au mlipe kidogo kidogo msafishaji hadi una maliza.
3. Uliza gharama za mawe, mchanga na cement pamoja na kujenga msingi. Anza kuweka mawe kulingana na kipato. Kisha mchanga na baadae nunua cement. Vikikamilika tafuta hela ya fundi fanya mambo.
4. Uliza matofali kiasi gani. Shuhulika na matofali mpaka yakamilike. Tafuta cement yake ya kujengea na hela ya fundi fanya mambo.
5. Nenda kwenye lenta nayo fanya hivyohivyo.
Hapo ni kwa ufupi naamini utanielewa. Ila kama unaweza, jichange ununue cement nyingi kwa wakati mmoja kwa maana ya msingi na kujengea maana cement inapanda bei kila uchao.
Mie nilijenga wakati kipato changu kikiwa laki 4 kwa mwezi. Toka kipande zaidi ya milioni sijafanikiwa hata kununua baiskeli.
Kwahiyo pamoja na kuwa kipato ni muhimu ktk ujenzi, lakini malengo na nia ndio muhimu zaidi. Na mara nyingi ukishaanza ujenzi, raha na faraja unazopata hakuna mtu atakushauri ubane matumizi. Kila ukipata hela utakua unakimbilia kutimiza kitu fulani kwy ujenzi.
Jinsi nyumba inavyopiga hatua...ndivyo hata mashavu yataanza kunona kutokana na amani na furaha unayoipata.
Kila la kheri!