Kwa mshahara wa laki saba naweza kujenga nyumba?

Cementi mfuko 18000
Nondo ya bei ya chini 22000
Mchanga lori 120000
Kumtizama fundi millioni.
Anyway nisikukatishe tamaa
 
Mkuu hata mshahara wa laki nne unaweza kujenga, mm nina nyumba 2 na viwanja 2 havijajengwa na nina mshahara kama wako, natembelea gari pia
Hapana mkuu labda uwe na marupurupu mengine. Miaka 9 iliopita niliwahi kulipwa hio laki saba baada ya matumizi yote nilikua nabaki na kama na laki moja hivi.
 
Cementi mfuko 18000
Nondo ya bei ya chini 22000
Mchanga lori 120000
Kumtizama fundi millioni.
Anyway nisikukatishe tamaa
Wapi huko..
Nilipo mimi cement 16,500 wanakuletea hadi unakojengea hatakama ni moja..

Lori kubwa la mchanga ni 70,000

Uwanja mita 25 Kwa 18 mil 2.5 kilomita 9 kutoka main road mjini kabisa..

Jamani tusing'ang'ane kujenga mjini daslaam tujenge hata mikoani tunapotoka, ukijenga unaweza pangisha nyumba yako then ikakulipa kodi huko unakofanya shughuli zako..

Lengo ukipata majanga msiba waweza kwenda kufanyika kwako kuondokana na viaibu vidogo vidogo Kwa familia na pengine angalau kuwaachia wanao baadae sio kuja kuteseka wakati we haupo.
 

Kaka Slim5 nilipokuwa nnafanya kazi dar dereva wa kampuni (mshahara 350,000) alikuwa na nyumba moja na anahangaika kumaliza ya pili. Kigamboni nilimuona mama mmoja wa makamo muuza matunda kwenye mabeseni posta anajenga banda zuri la vyumba vitatu. Mjini mipango kweli.
 
Habari za majukumu wakuu,

Naomba mwenye ujuzi na uzoefu juu ya masuala ya ujenzi anisaidie. Nahtaji kujenga nyumba ya vyumba vitatu kiwanja tayari ninacho na mshahara wangu ni laki 7 kwa mwezi.

Asante na karibuni
Utajenga nyingi mno+maisha mazuri sana...kama ukiapply hii theory

the state to be a rich is not what you gain,but what you save


Y=C+S
 
mkuu nimekuelewa mnoo
 
Habari za majukumu wakuu,

Naomba mwenye ujuzi na uzoefu juu ya masuala ya ujenzi anisaidie. Nahtaji kujenga nyumba ya vyumba vitatu kiwanja tayari ninacho na mshahara wangu ni laki 7 kwa mwezi.

Asante na karibuni
Unaweza.
Kila mwezi, nunua matofali mia mbili ambayo ni kama Tsh laki mbili na nusu kisha peleka site. Mpaka mwaka mmoja unaisha utakuwa na matofali 2400.
Hayo yanatosha sana kujenga nyumba ndogo ya vyumba vitatu. Yasipotosha, utahitajika kuongezea kidogo...
 
anzisha mradi kwanza faida unayoipata ingiza kwenye ujenzu, usikope kwa ajili ya kujenga
mkuu mbona umewaza hivyo tupe maelezo kidogo na ushuhuda ikiwezekana[emoji23]
 
anzisha mradi kwanza faida unayoipata ingiza kwenye ujenzu, usikope kwa ajili ya kujenga
Hiii sitosahau mkuu, nilikurupuka kufanya hivi nikashindwa kumaliza nyumba, ikabidi niishi ivoIvo
 
Ninamfahamu secretary mmoja serikalini analipwa 390,000/ sijui ni kabla au baada ya makato amejenga nyumba japo ametumia km miaka minne mitano hivi. Kamaliza, na alinambia hajajengewa na mtu.

So ni wewe tu namna ya kujipanga!
Unawajua masekretari wewe? Bosi kachangia hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…