The Crushing
JF-Expert Member
- Apr 27, 2018
- 569
- 903
Jibu Ni ndio unaweza
Watu mmeulizwa swali dogo mnaleta maelezo kibao
Watu mmeulizwa swali dogo mnaleta maelezo kibao
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapana mkuu labda uwe na marupurupu mengine. Miaka 9 iliopita niliwahi kulipwa hio laki saba baada ya matumizi yote nilikua nabaki na kama na laki moja hivi.Mkuu hata mshahara wa laki nne unaweza kujenga, mm nina nyumba 2 na viwanja 2 havijajengwa na nina mshahara kama wako, natembelea gari pia
Wapi huko..Cementi mfuko 18000
Nondo ya bei ya chini 22000
Mchanga lori 120000
Kumtizama fundi millioni.
Anyway nisikukatishe tamaa
mtaani kuna fundi viatu anajenga nyumba..... kuna jamaa angu alikuwa anauza viwanja vyake, nikawa namsaidia kuvitangaza... kuna siku nilienda kumsaidia zoezi la mauziano... mmoja wa wateja wake ni mshkaji dereva wa bajaj kituo cha mtaani.... kuna siku ktk dala dala ya STESHENI - MAKUMBUSHO nilimskia konda anamfokea engineer (mi nilielewa fundi wake) baada ya engineer kumwambia siku hiyo hawatafanya kazi, vibarua hawajatokea site! Nimejifunza Mjini Mipango na usithubutu kujua mipango ya watu!
Utajenga nyingi mno+maisha mazuri sana...kama ukiapply hii theoryHabari za majukumu wakuu,
Naomba mwenye ujuzi na uzoefu juu ya masuala ya ujenzi anisaidie. Nahtaji kujenga nyumba ya vyumba vitatu kiwanja tayari ninacho na mshahara wangu ni laki 7 kwa mwezi.
Asante na karibuni
mkuu nimekuelewa mnooPamoja na ushauri wote wa mapato na matumizi, kibongobongo wengi wetu tumejenga kwa kuangalia hitaji la wakati husika.
Ushauri wangu ni kuwa Ujenzi wetu wa kipato cha chini huo tunaufanya kwa kugawanya hatua za ujenzi katika awamu kama ifuatavyo:
1. Anza kununua mabati.
Hii ni muhimu sana maana nyumba ikisha pauliwa inatakiwa iezekwe haraka vinginevyo mbao za paa zitapinda.
2. Uliza gharama za kusafisha uwanja. Ukipata changa pesa au mlipe kidogo kidogo msafishaji hadi una maliza.
3. Uliza gharama za mawe, mchanga na cement pamoja na kujenga msingi. Anza kuweka mawe kulingana na kipato. Kisha mchanga na baadae nunua cement. Vikikamilika tafuta hela ya fundi fanya mambo.
4. Uliza matofali kiasi gani. Shuhulika na matofali mpaka yakamilike. Tafuta cement yake ya kujengea na hela ya fundi fanya mambo.
5. Nenda kwenye lenta nayo fanya hivyohivyo.
Hapo ni kwa ufupi naamini utanielewa. Ila kama unaweza, jichange ununue cement nyingi kwa wakati mmoja kwa maana ya msingi na kujengea maana cement inapanda bei kila uchao.
Mie nilijenga wakati kipato changu kikiwa laki 4 kwa mwezi. Toka kipande zaidi ya milioni sijafanikiwa hata kununua baiskeli.
Kwahiyo pamoja na kuwa kipato ni muhimu ktk ujenzi, lakini malengo na nia ndio muhimu zaidi. Na mara nyingi ukishaanza ujenzi, raha na faraja unazopata hakuna mtu atakushauri ubane matumizi. Kila ukipata hela utakua unakimbilia kutimiza kitu fulani kwy ujenzi.
Jinsi nyumba inavyopiga hatua...ndivyo hata mashavu yataanza kunona kutokana na amani na furaha unayoipata.
Kila la kheri!
Unaweza.Habari za majukumu wakuu,
Naomba mwenye ujuzi na uzoefu juu ya masuala ya ujenzi anisaidie. Nahtaji kujenga nyumba ya vyumba vitatu kiwanja tayari ninacho na mshahara wangu ni laki 7 kwa mwezi.
Asante na karibuni
mkuu mbona umewaza hivyo tupe maelezo kidogo na ushuhuda ikiwezekana[emoji23]anzisha mradi kwanza faida unayoipata ingiza kwenye ujenzu, usikope kwa ajili ya kujenga
Kweli aiseeUsiamini vipato vya wanawake hususani ma secretary, wengi wana biashara ya siri na ma bosi...ukijilinganisha nao utaanga town jomba
Unawajua masekretari wewe? Bosi kachangia hapo.Ninamfahamu secretary mmoja serikalini analipwa 390,000/ sijui ni kabla au baada ya makato amejenga nyumba japo ametumia km miaka minne mitano hivi. Kamaliza, na alinambia hajajengewa na mtu.
So ni wewe tu namna ya kujipanga!