Tukiachana na ushabiki wa uyanga wangu, huyu Baleke Simba wamepata mtu mwenye shabaha na nyavu zilipo. Huyu jamaa kaja katikati ya msimu ila alichokionesha uwanjani kitakwimu zinaogopesha sana wapinzani. Tunaweza kuongea kiushabiki tu kuwa kazifunga timu ndogo, lakini tujiulize hizi timu ndogo au dhaifu Mayele pia anakutana nazo lakini Kwanini hazifungi goli 2+?
Sijui kipengele cha utaratibu wa usajili wa mkopo upoje, kwamba mchezaji akipelekwa timu kwa miaka miwili n lazima aitumikie au timu iliyompeleka kwa mkopo wanaweza kumrejesha kikosini muda wowote wakimtaka. Wajuzi mtanifahamisha hilo kama ipo hivyo basi Simba kwasasa ni muda sahihi wa kuangalia namna ya kupata umiliki halali wa huyu mwamba ameonesha kitu kikubwa sana halafu kwa muda mchache sana.
Pamoja na kulia aliye waletea Sawadogo, basi mumshukuru sana kwa huyu Baleke