Kwa msimu wa 2022/23 Yanga imepata hasara ya zaidi ya Tsh. Bilioni 4

Kwa msimu wa 2022/23 Yanga imepata hasara ya zaidi ya Tsh. Bilioni 4

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Kama mnavyojua weekend iliyopita klabu ya Yanga ilifanya mkutano mkuu wa wanachama wake na moja ya ajenda ya mkutano ilikuwa kutoa ripoti ya mapato na matumizi ya mwaka 2022-2023.

Kumezuka mjadala mkubwa ambao nadhani na mimi nimechangia sana kuuleta wa kuhoji taarifa zilizokuwa zinasambaa kuwa Yanga imepata FAIDA ya 500M. Jana katika uzi mmoja nilikuwa na majadiliano marefu na Tsh na kuna jambo moja niligusia kwamba inawezekana tulichoonyeshwa siyo ripoti ya faida/hasara bali ni ripoti ya mzunguko wa fedha, yaani pesa zilizoingia na kutoka ndani ya mwaka huu. Hii ni tofauti kubwa sana katika mahesabu ya kihasibu. Nakumbuka kugusia kuwa tulichoonyeshwa ni Statement of Cash Flow na siyo Income Statement, kwa wale walio na ufahamu na mambo ya kihasibu watanielewa hivi vitabu vina kazi gani.

Leo nimeenda tena kusikiliza kwa makini ripoti ile na nikiri kuwa nimepata maelezo zaidi ya yale niliyokuwa nayo jana. Mfano jana niliishutumu Yanga kuwa hawakutoa taarifa ya marejesho ya mkopo wa 4.8 B wala malipo ya riba au gharama nyingine za kupata mkopo ule. Baada ya kusikiliza tena inaonyesha hayo malipo yamefanyika ila kwa kiwango kidogo (marejesho ya mkopo ni 38M na malipo ya riba na gharama za kifedha ni 120M) kwa hiyo nadhani huu mkopo hauna muda mrefu toka ulivyochukuliwa. Kwa hili naomba radhi kwa usumbufu wowote uliotokea kwa wahusika.

Bado ripoti ile ina mapungufu, mfano kuna gharama ambazo tunajua Yanga imeziingia msimu huu lakini hazijaorodheshwa na pia kuna gharama zingine zinazoonekana kufanana zimeorodheshwa zaidi ya mara moja. Hilo nitaliacha kwa sasa.

Pamoja na hayo, taarifa zilizokuwa zinasambazwa hasa na wapenzi wa Yanga kuwa Yanga imepata FAIDA ya 500M bado siyo sahihi. Kwanza inaonyesha mtoa taarifa wakati wa Mkutano Mkuu, Bw. Sabri, Mkurugenzi wa Mambo ya Fedha wa Yanga hakusema kuwa 500M ni faida. Hili sasa si kosa lake bali ni kosa la waliosambaza taarifa hadi kuleta hii mijadala na sintofahamu. Alichosema Sabri ni kuwa ile ni balance ya pesa iliyobaki mikononi mwao hadi mwishoni mwa mwaka wa fedha na hii kihasibu ni tofauti na FAIDA.

Ukitaka upate estimation ya faida iliyopatikana msimu huu (tukifanya assumption kuwa mapato na matumizi yote yaliyoorodheshwa yanahusiana na mwaka huu wa fedha wa Yanga na siyo ya misimu ya nyuma au msimu ujao maana mfumo wa kihasibu wa "Accrual" itabidi kutoa au kuongeza baadhi ya gharama au mapato kutoka katika mahesabu haya kulingana na mwaka ambao yanahusika), basi moja ya item kubwa ambayo inatakiwa kuondolewa ni mapokeo na marejesho ya mkopo wa ile 4.8 Billion na hili nililisema na kulisisitiza sana jana na hapa bado niko sahihi. Pia inabidi gharama za riba na nyingine za kifedha ziendelee kujumuishwa. Ukifanya hayo yote unakuta Yanga wamepata hasara ya karibia Bilioni 4.

Tsh

CC: BODI YA TAIFA YA WAHASIBU NA WAKAGUZI WA HESABU TANZANIA (NBAA), PwC
 
Mwaka huu Yanga wamewaweza kila kona.

Anyway next season bajeti ni Bilion 20.
 
Back
Top Bottom