Kwa mtaji wa milioni moja naweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa milioni moja naweza kufanya biashara gani?

Zombie S2KIZZY

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2021
Posts
826
Reaction score
1,622
Wakuu habari,

Nisaidien kitu Hapa hivi kwa mtaji wa million moja nawezafanya biashara ipi wakuu
 
Upo mkoa gan,jinsia gani na una elimu gan
 
Kama unataka biashara za kuonekana basi hii yangu usifanye ila kama unachohitaji ni pesa iingie kila siku fanya hivi

Tafuta vijana watano fungua vijiwe vitano kaanga kuku wa kisasa kwenye meza kila meza kuku kumi waishe kwa siku hapa kaanga kuku tu achana na habari ya viazi kuku mmoja kwa wafugaji sasa hivi anauzwa 6500 na kwa sokoni ni 7000

Ukishamchinja na kumkata vipande mchanganuo huwa uko hivi:-

Vidali viwili @2500x2=5000

Mapaja mawili @2000x2=4000

Utumbo hufungwa pamoja na firigisi @800

Kichwa 300

Miguu miwili @100x2=200

JUMLA (5000+4000+800+300+200)=10300

10300-7000=3300 ambayo ni faida ya kuku mmoja

Kila kijiwe uza kuku kumi tu kwa siku hapo utazidisha mwenywe faida yake

Kuhusu mafuta utakayonunua siku unaanza biashara utakuwa hununui kila siku maana kuku wenyewe huwa wanazalisha mafuta hivyo mpaka uamue uyabadilishe kwa kuyamwaga na kununua mapya

Jiko tumia gesi achana na mikaa

Hakikisha meza iko maeneo ambayo wanapita watu wengi hasa jioni

Biashara anza mapema hasa saa kumi jioni utarudi kunishukuru
 
Back
Top Bottom