Kama unataka biashara za kuonekana basi hii yangu usifanye ila kama unachohitaji ni pesa iingie kila siku fanya hivi
Tafuta vijana watano fungua vijiwe vitano kaanga kuku wa kisasa kwenye meza kila meza kuku kumi waishe kwa siku hapa kaanga kuku tu achana na habari ya viazi kuku mmoja kwa wafugaji sasa hivi anauzwa 6500 na kwa sokoni ni 7000
Ukishamchinja na kumkata vipande mchanganuo huwa uko hivi:-
Vidali viwili @2500x2=5000
Mapaja mawili @2000x2=4000
Utumbo hufungwa pamoja na firigisi @800
Kichwa
300
Miguu miwili @100x2=200
JUMLA (5000+4000+800+300+200)=10300
10300-7000=3300 ambayo ni faida ya kuku mmoja
Kila kijiwe uza kuku kumi tu kwa siku hapo utazidisha mwenywe faida yake
Kuhusu mafuta utakayonunua siku unaanza biashara utakuwa hununui kila siku maana kuku wenyewe huwa wanazalisha mafuta hivyo mpaka uamue uyabadilishe kwa kuyamwaga na kununua mapya
Jiko tumia gesi achana na mikaa
Hakikisha meza iko maeneo ambayo wanapita watu wengi hasa jioni
Biashara anza mapema hasa saa kumi jioni utarudi kunishukuru