Kwa mtaji wa Tsh 150, 000

Kwa mtaji wa Tsh 150, 000

honey bee

Senior Member
Joined
Nov 23, 2021
Posts
139
Reaction score
232
Naomba kuuliza,
Hivi kwa mtaji wa sh laki moja na nusu, naweza anzisha biashara gani inayolipa na yenye uwezo wa kunipatia faida ya hadi 20, 000 kwa siku!
Msaada tafadhari!!
Lakini isiwe network money ya tuma link!!
 
Uza mkaa wa mafungu au hereni zile za buku tunazouziwa buku mbili.Mkaa chukua ule wa debe 1 buku 3 then sisi tunauziwa buku 6
 
Naomba kuuliza,
Hivi kwa mtaji wa sh laki moja na nusu, naweza anzisha biashara gani inayolipa na yenye uwezo wa kunipatia faida ya hadi 20, 000 kwa siku!
Msaada tafadhari!!
Lakini isiwe network money ya tuma link!!
Uza lamba lamba mashuleni.
 
Peleka Ukraine zikasaidie wahanga wa vita vya Mmarekani na NATO
 
Naomba kuuliza,
Hivi kwa mtaji wa sh laki moja na nusu, naweza anzisha biashara gani inayolipa na yenye uwezo wa kunipatia faida ya hadi 20, 000 kwa siku!
Msaada tafadhari!!
Lakini isiwe network money ya tuma link!!
Kama upo dar,,,
Nenda mitaa yenye watu wengi jioni kauze pweza kachori na supu ya pweza

Nenda feri nunua pweza kwa kilo nazani haizidi elf 12 tafta jiko vikombe mkaa chupa za chai meza nk anza kuuza but mwanzoni itakupa shida but vumilia

Kabla ya yote tembelea wauzaji kama watano wafanyie research wakupe ABC na wakufundishe jinsi ya kuandaa pweza

Nb tafta eneo lenye watu wengi uza kuanzia SAA 12 jion
 
Kwa mtaji wa laki na nusu inaweza Fanya biashara gani??(taja na mahali unapochukulia hiyo biashara ni wapi).
Je inaweza fanikiwa ukawa mtaji mkubwa kabisa?
 
Kwa mtaji wa laki na nusu inaweza Fanya biashara gani??(taja na mahali unapochukulia hiyo biashara ni wapi).
Je inaweza fanikiwa ukawa mtaji mkubwa kabisa?
Oil chafu
Mifuko ya Jafafa ana aina nyinginezo
Mapipa ya viwandani ya plastic na ya Bati
Na waste kibao tuu.. Ukishatengeneza mtandao wako biashara itakuwa maradufu
 
hapa ndo utasikia nilianza na kuku watatu Sasa hivi Nina kuku 300.
 
Kwa mtaji wa laki na nusu inaweza Fanya biashara gani??(taja na mahali unapochukulia hiyo biashara ni wapi).
Je inaweza fanikiwa ukawa mtaji mkubwa kabisa?
150,000 inategemea wewe ni binti wa aina gani
Ila viatu vya kike vinaweza kukusogeza uza online nenda kachukue kwa order fanya kila kiatu weka faida buku tatu (3000) na delivery weka 3000 hadi 5000 kulingana na umbali kama unahitaji muongozo zaidi kuhusu biashara hii niulize hapa chochote
 
S

Shusha elimu
Oil chafu inaingia kwenye malighafi taka (taka taka ama waste) hii ni bidhaa yenye matumizi mengi yasiyopewa kipaumbele na wengi
Ni dawa ya wadudu majumbani
Inadhibiti harufu vyooni
Ni chanzo mbadala cha nishati viwandani
Ni kilaishi
Kwa sasa lita moja ya oil chafu imepanda toka mia tatu na mia nne hadi kufikia 700 mpaka 1000 kulingana na ubora
Uwekezaji wake sio mkubwa, na mara nyingi huhitaji kukodi eneo bali hata mahali unapoishi ama kijiweni kwa mshkaji unaweza kuweka pipa lako la lita 1000 na kuweka tangazo la kununua oil chafu

Upatikanaji wake ni kwenye vijiwe vya service za bodabida, magereji, na service stations kwenye vituo vya mafuta ama makampuni, bandarini na mahali kunakohifadhiwa mafuta mengi kwenye matank makubwa

BUKOBA LAND
 
Back
Top Bottom