afanye biashara ya nguo za mtumba za kupoint sio belo (kupunguza risk ya kupata mzigo mbaya) ilala boma na karume ndio kuzuri ilala boma nguo zinaanzia 1500, 2000 hiyo ni kwa shiffon blouse,masweta mazuri,top etc... skin jenas 3000 na 4000 na magauni mazuri ni 2000 na 3000....anapoint ananyosha anaingiza sokoni kwa bei ua elfu 6000 tu hadi 7000 atapata pesa akiifanya kaka machinga aachane na frame.....
**** biashara ya kutengeneza bahasha za kaki hii inalipa kama eneo lako halijapata huduma hii...hapo ela ni kaki zenyewe na gundi ya maji....
**** biashara ya kuku wa kienyeji kuifanya kwa kutoa vijijini na kuweka mjini, na kuwakuza alafu kipindi cha sikukuu unawauza....ila hii ni changamoto sana hasa sehem ya kufugia....
Kununua nguo za ndani za kina dada na kuzizungusha majimbani na saloon etc dozen zake zinapatikana kariakoo kwa quality mbalimbali.....
Kuchoma mishikaki na kuuza stand za mabasi ukizingatia usafi na njia bora ya uchomaji utapata hata 25000 kwa siku....
Kuna biashara ya kukaanga mihogo na kuku wa kisasa na kumkata vipande vya 500 tu viwe vingi kukuletea 12000 maana kuku wa nyama ni 6000 hadi 6500....mihogo sijajua ulipo kata midogo kiasi uza 200 kaanga vizuri, unaweza jifunza kukaanga viazi vya mayai (vnavyotumia ngano) vnauza pia.....watu mtaani wavivu kupika hizo ndio menu zao
Unaweza kuwa unafanya biashara ya kusambaza bidhaa madukani kama mikate, mayai, dagaa etc....hautatoka mtupu mkuu....
hiyo biashara ya nguo nilikuwa naingiza elfu 50000 kwa mtaji wa 250000 ila hapo 22 ni mtaji 28 ndio ya kula na mambo mengine nikaacha sababu ya ajira ila ni profitable business hasa kwa nguo za wadada