Kwa mtaji wa Tsh. 400,000/- naweza fanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Tsh. 400,000/- naweza fanya biashara gani?

afanye biashara ya nguo za mtumba za kupoint sio belo (kupunguza risk ya kupata mzigo mbaya) ilala boma na karume ndio kuzuri ilala boma nguo zinaanzia 1500, 2000 hiyo ni kwa shiffon blouse,masweta mazuri,top etc... skin jenas 3000 na 4000 na magauni mazuri ni 2000 na 3000....anapoint ananyosha anaingiza sokoni kwa bei ua elfu 6000 tu hadi 7000 atapata pesa akiifanya kaka machinga aachane na frame.....

**** biashara ya kutengeneza bahasha za kaki hii inalipa kama eneo lako halijapata huduma hii...hapo ela ni kaki zenyewe na gundi ya maji....

**** biashara ya kuku wa kienyeji kuifanya kwa kutoa vijijini na kuweka mjini, na kuwakuza alafu kipindi cha sikukuu unawauza....ila hii ni changamoto sana hasa sehem ya kufugia....

Kununua nguo za ndani za kina dada na kuzizungusha majimbani na saloon etc dozen zake zinapatikana kariakoo kwa quality mbalimbali.....

Kuchoma mishikaki na kuuza stand za mabasi ukizingatia usafi na njia bora ya uchomaji utapata hata 25000 kwa siku....

Kuna biashara ya kukaanga mihogo na kuku wa kisasa na kumkata vipande vya 500 tu viwe vingi kukuletea 12000 maana kuku wa nyama ni 6000 hadi 6500....mihogo sijajua ulipo kata midogo kiasi uza 200 kaanga vizuri, unaweza jifunza kukaanga viazi vya mayai (vnavyotumia ngano) vnauza pia.....watu mtaani wavivu kupika hizo ndio menu zao

Unaweza kuwa unafanya biashara ya kusambaza bidhaa madukani kama mikate, mayai, dagaa etc....hautatoka mtupu mkuu....

hiyo biashara ya nguo nilikuwa naingiza elfu 50000 kwa mtaji wa 250000 ila hapo 22 ni mtaji 28 ndio ya kula na mambo mengine nikaacha sababu ya ajira ila ni profitable business hasa kwa nguo za wadada
Naipenda sana biashara ya nguo na viatu, tatizo sizielewi bado zipi kali kwamba nayochukua ni nzuri kuliko nayoacha
 
Mimi ni mjasiliamali nimepita kwenye biashara nyingi sana najua faida na hasara hivyo basi mwenye dukuduku kuhusu pembejeo za kilimo na mifugo,Uchomaji wa kuku,Biashara za matunda n.k anicheki tutashilikiana kimawazo kwa pamoja tunaweza
 
Kama upo maeneo ya kanda ya ziwa nenda kisiwa kimoja kinaitwa Goziba kusanya samaki mzigo ukiwa mkubwa nenda kauze samaki na bondo. Hiyo 400,000 nakuhakikishia kwa wiki utapata zaidi ya 100,000 faida.

Ukiachana na hiyo ya samaki chukua dagaa kauzie mwaloni kirumba kakusanye huko bukoba na hii utakuja kutoa ushuhuda hapa tena kuhusiana na dagaa nitafute nikupe maelekezo yote make nailewa sana.

Nenda ushirombo au Simiyu kusanya kuku wa kienyeji afu uje kuuza Mwanza mjini kwa bei ya jumla. Man biashara ipo nyingi sana. But deal na chakula kwa muda huu
tafadhali nipe bei ya dagaa debe wale dagaa wasio na mchanga
 
Mkuu shukrani sana maana hii biashara ya nguo za mtumba za kike nataka niianze pia pesa sio shida shida ni mda tu maana ni muajiriwa. ukiachana na ilala boma Chimbo gani linakuwaga na nguo za kuchagua kwa bei hiyo?? vp karume muda huo vipi?
karume ndio mambo yote kwa mtumba tz
 
Hizi khaki ni zile vijana wetu wanajaladia madaftari ama kuna zinapouzwa spesheli
Wanatengeneza hivo mkuu....ukiongeza kamba za katani kwa juu kwa package kubwa inakuwa nzuri....kwa ndogo acha hvohvo tu.....hakikisha zinakuwa na ukubwa mbalimbali nyingi ziwe na ule ukubwa wa rambo za 100 zamani....

Ukishindwa elewa hizo picha, jaribu kugoogle how to create paper bag youtube au kwa kiswhaili jinsi ya kutengeneza mifuko ya kaki/vifungashio vya kakiView attachment 1726604
 
Back
Top Bottom