Kwa mtazamo wa Kidini. Je, mwanamke anaweza kuwa Rais?

Poppy Hatonn

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2021
Posts
3,095
Reaction score
4,632
Kwa sasa, tunaona mwanamke anayewania urais pamoja na chama cha siasa kinachotaka mgombea wao wa nafasi hiyo awe mwanamke.

Hata hivyo, dini inasema bila utata kwamba mwanamke haruhusiwi kuwa kiongozi mkuu wa nchi. Anaweza kuwa makamu wa rais, waziri, au kushika nafasi nyingine za uongozi, lakini si kuwa mkuu wa dola.

Kwa muktadha huo, tunaposema mwanamke anaweza kuwa rais, tunapingana na maandiko matakatifu tuliyo nayo.

Sasa tunafanyaje?

Katika Biblia, kuna hadithi ya mfalme aliyesema, "Siku nyingi hekalu halijakarabatiwa. Nataka hekalu likarabatiwe." Wakati wa ukarabati, walikuta kitabu cha Torati. Waliposoma maandiko yake, mfalme aligundua kuwa taifa lilikuwa linafanya mambo mengi yaliyokatazwa. Akauliza, "Tufanye nini sasa?"

Je, Watanzania tunapaswa kujiuliza swali hilo hilo?

Ikumbukwe kuwa Ikulu ilipojengwa awali, haikuwa nyumba ya mtawala; ilikuwa chuo cha dini ya Kiislamu. Sasa, tunajadili jambo ambalo limekatazwa katika Msahafu.

Tunasema mwanamke anaweza kuwa rais, lakini Msahafu unakataa.

Kwa mfano, hata Kanisa Katoliki limekataa kuwapa wanawake upadrisho, na suala la wanawake kuwa maimamu bado halijakubaliwa.

Pengine ni wakati wa kurudi kwenye misingi ya imani na historia ya taifa letu.
 
 

Attachments

  • 5952631-0291b2ca9c7d3b297e2c695a9fc8f5a7.mp4
    4.5 MB
Kwa hiyo SSH hafahamu hayo yaliyomo kwenye kitabu chenu??? Maana angekuwa ni Mgalatia angeweza kusema hiyo Quran haimuhusu.
 
Video moja nimeiweka jana mod ameiondoa; wanawake Uswahilini wameandaa Ngoma wanacheza wanasema hawamtaki Mama Samia.
Anaulizwa yule demu huku,huku anachrza Ngoma;
Q: Unaitwa nani?
A; Naitwa Saradeo mtoto wa Kimakonde.....
(Shangwe)
Q: Sababu ya kutokumtaka Mama Samia ni nini?
A; Mama Samia huyu huyu mkorofi.
Mama Samia huyu huyu tapeli wa mitandaoni.
( Shangwe).
 
Hawa mods ni wapuuzi sana. Kiufupi ni mamluki.

Jana kuna uzi nimepandisha hata haikupita dakika wakawa wameufuta like wtf.!!
 
Umesema anaweza kuwa makamu na katiba inasema Rais akitangulia makamu anashika nchi
 
Zanzibar karibu 99% ni waislam na kwenye dini Yao Mwanamke hafai kuwa kiongozi na kiasi flani anadharauliwa sana, kutokana na haya Samia anajitahidi kufanya Kila analoweza kujenga mabarabara mpaka vichochoroni, ujenzi wa masoko ya kisasa Kila wilaya, ujenzi wa mahospitali makubwa nk haya yote Ili kuwaonyesha jamii ya kizanzibar kwamba kuliwahi kutokea Rais Mwanamke aliyefanya mambo makubwa kuliko hao Marais wanaume waliopita
 
na watu hawastuki mambo yanaenda kombo
 
Dini gani hiyo unayozungumzia?
 
Tumia akili,uraisi sio mambo ya dini.Mama ako aliongoza,nyumba yenu,hata baba ako,anajua hilo.
 
Dini ipi hiyo? Usitulazimishie imani yako. Hii dini ya Afghanistan? Acha kuiga kunya kwa tembo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…