Hamku liona hilo mlipoweka Katiba kwamba ikitokea maradhi au kifo Makamu wa Raisi anachukua Madaraka. Kwani hakuna viongozi wakubwa Ndani ya Serikali na kwenye chama hakuna aliye muislamu au mkristo wa Torati.Kwa sasa, tunaona mwanamke anayewania urais pamoja na chama cha siasa kinachotaka mgombea wao wa nafasi hiyo awe mwanamke.
Hata hivyo, dini inasema bila utata kwamba mwanamke haruhusiwi kuwa kiongozi mkuu wa nchi. Anaweza kuwa makamu wa rais, waziri, au kushika nafasi nyingine za uongozi, lakini si kuwa mkuu wa dola.
Kwa muktadha huo, tunaposema mwanamke anaweza kuwa rais, tunapingana na maandiko matakatifu tuliyo nayo.
Sasa tunafanyaje?
Katika Biblia, kuna hadithi ya mfalme aliyesema, "Siku nyingi hekalu halijakarabatiwa. Nataka hekalu likarabatiwe." Wakati wa ukarabati, walikuta kitabu cha Torati. Waliposoma maandiko yake, mfalme aligundua kuwa taifa lilikuwa linafanya mambo mengi yaliyokatazwa. Akauliza, "Tufanye nini sasa?"
Je, Watanzania tunapaswa kujiuliza swali hilo hilo?
Ikumbukwe kuwa Ikulu ilipojengwa awali, haikuwa nyumba ya mtawala; ilikuwa chuo cha dini ya Kiislamu. Sasa, tunajadili jambo ambalo limekatazwa katika Msahafu.
Tunasema mwanamke anaweza kuwa rais, lakini Msahafu unakataa.
Kwa mfano, hata Kanisa Katoliki limekataa kuwapa wanawake upadrisho, na suala la wanawake kuwa maimamu bado halijakubaliwa.
Pengine ni wakati wa kurudi kwenye misingi ya imani na historia ya taifa letu.
Na walioabdika Katiba ni wanasiasa au wanasheria , hawa kufanya rejea ya vitabu vya dini . Viongozi wa Dini zetu hawakuhusishwa. Walidharauliwa.
Hivi viongozi wetu wa chama na sirikali, hawaombi ushauri toka Kwa Bagonza au Kitime au Ponda.
Nini matumizi ya kamati ya Amani, ni kusamehe na kuwadanganya raia wawasamehe viongozi waongo na wezi ili watuibie vizuri na sio kutenda haki.