Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Polybius, Mwanafilosofia wa kale wa Ugiriki na baadaye mfungwa wa Roma kisiasa aliyeishi karne ya pili kabla ya Kristo alichukua muda mrefu kujifunza mifumo ya serikali na historia yake katika nchi yake ya Ugiriki na Utawala wa Roma akaja na nadharia maarufu ya "anacyclosis".
Katika nadharia ya anacyclosis Polybius anasema tawala zote zilizopevuka kisiasa huwa zinaptia mzunguko wa aina tatu(3) za serikali. Ya kwanza ni Ufalme, ya pili Aristocracy(tabaka la watu wachache mahiri na wazalendo) na ya tatu,.Demokrasia ya uwakilishi.
Anasema huu ni mzunguko naturally ambapo kila aina ya mfumo mmoja wa serikali huwa unaondolewa na kupisha mwingine naturally. Kwamba Tawala za kifalme huwa zinaanza vizuri baada ya miaka kadhaa warithi wanageuka makatili na mafisadi kwa raia wao(tyranny) ndipo kunatokea maasi watu wachache mahiri(aristocrats) wanapata nguvu juu ya ufalame. Aristocrats nao hugeuka mafisadi na incompetents (oligarchs) ndipo raia wanawachoka na kuweka Demokrasia. Baada ya muda katika demokrasia napo inafika wakati utawala wa majority unakuwa unafanya maamuzi ya kipumbavu na hovyo tu hadi kupeleka kuibuka kwa populists demagogues na baadaye mob rule.
Ukiangalia huu mzunguko Africa ni kama tumejaribu kurukia demokrasia moja kwa moja labda ndio maana inakuwa vigumu sana kujielewa na kupata uongozi thabiti. Huenda tuliharakishwa kukimbia kabla ya kuanza kutambaa.