Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Au agenda iliyopo sasa ni kuwatembelea viongozi wastaafu tu?
Maana kazi kubwa mpaka sasa ambayo inafanyika ni ile ambayo wataalamu na wachambuzi wengi wa siasa za vyama vya siasa Tanzania walitarajia, kazi ya kuwavua uanachama, kuwaengua kwa fedheha viongozi watendaji wa chadema waliokua chini ya uongozi wa mwenyekiti wa zamani, jambo ambalo linazidisha na kuendeleza uhasama, chuki na migawanyiko zaidi miongoni mwa wanachadema wa kambi zilizokua zinawania uongozi wa chadema kitaifa.
Matarijio mengine ambayo wabobevu wa siasa za Tanzania waliangazia kuyaoni yakichochewa na kusababishwa na uongozi mpya wa chadema, ni pamoja na baadhi ya viongozi mbalimbali wa chadema kujiengua kwa hiyari zao na kujiunga na vyama vingine kukwepa siasa za fujo zilizokosa ustaarabu, maandamano, migomo, matamko na press conference zisizo na tija, vitu ambavyo vimewekwa kama vipaumbele muhimu vya uongozi mpya wa chadema.
Kipaumbele cha chadema kwa sasa ni kuwaengua uanachama wanachama wake hasa wale waliokua wanamuunga mkono kiongozi wa zamani wa chadema taifa kwa chuki na hila hila binafsi, kuwasimamisha na kufukuza uanachama wale wote wenye mawazo tofauti na ile ya mwenyekiti halafu kwenye media wanadaini ni uhuru wa kutoa maoni.
Nini mtazamo wako kama mdau wa demokrasia za vyama vya siasa nchini?
Mungu Ibariki Tanzania